Majira ya kupuputika majani
msimu unaofuata baada ya majira ya joto na msimu kabla ya msimu wa baridi
(Elekezwa kutoka Masika)
Majira ya kupuputika majani (kwa Kiingereza Fall au Autumn)[1] ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kiasi. Kadiri ya umbali na ikweta, mchana unazidi kuwa mfupi na usiku kuwa mrefu.

Pamoja na hayo, miti mingi, isipokuwa misonobari na misanduku, inaweza ikapotewa na majani yote: ndiyo asili ya jina la majira.
Kwa Kiswahili majira ya namna hiyo pia huitwa masika.
Yanafuata majira ya joto (kwa Kiingereza "Summer") na kutangulia majira ya baridi (kwa Kiingereza "Winter").
Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.
Tanbihi hariri
- ↑ Oxford Dictionary on the North American usage of Fall. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-03-30. Iliwekwa mnamo 2015-04-04.
Viungo vya nje hariri
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- How To Photograph Autumn Color Archived 9 Mei 2013 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Majira ya kupuputika majani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |