Makaveli & Dillinger Don't Go 2 Sleep
Makaveli & Daz Dillinger Don't Go 2 Sleep - Tha EP ni albamu ya kutaja nyimbo mchanganyiko iliyotolewa na Makaveli na Daz Dillinger. Albamu hii ina nyimbo nane. Kuna matoleo mengine mawili ya (bootleg) ambayo pia ni EP, lakini toleo halisi lina nyimbo nane tu. Albamu ilitolewa mnamo tar. 24 Desemba, 2001 kupitia studio ya D.P.G. Recordz. Albamu zilirekodiwa katika studio za Death Row Records kati ya mwaka wa 1995-96 kwa ajili ya mradi wa Tupac na Boot Camp Clik "One Nation". Baadaye wakati Daz ameondoka Death Row, amekwiba baadhi ya nakala kuu ya kiasi cha nyimbo za Tupac ambazo hazijatolewa, baadhi zinaweza kusikika katika albamu hii ya EP. Wimbo pekee ambao umeachwa bila kuguswa na Daz ni "They Don't Give a Fucc About Us", lakini hizo nyingine alifanya remixi zake na kujiingiza kwenye nyimbo ambamo awali hakuwepo.
Don't Go 2 Sleep | |||||
---|---|---|---|---|---|
EP ya Makaveli | |||||
Imetolewa | Desemba 24, 2001 | ||||
Imerekodiwa | 1995-96 | ||||
Aina | Rap | ||||
Urefu | 48:33 | ||||
Lebo | D.P.G. Recordz | ||||
Mtayarishaji | Daz Dillinger | ||||
Wendo wa albamu za Makaveli | |||||
|
Makadirio ya kitaalamu | |
---|---|
Tahakiki za ushindi | |
Chanzo | Makadirio |
Worldwide Westside Magazine | [1] |
Marejeo
haririViungo vya Nje
hariri- westcoast2k Ilihifadhiwa 4 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- DPG Recordz Ilihifadhiwa 2 Juni 2013 kwenye Wayback Machine.
- Death Row Records Ilihifadhiwa 20 Julai 2006 kwenye Wayback Machine.
- Internet Wayback for archived pages