Makumbusho ya Karonga

Makumbusho ya Karonga (kirefu: Kituo cha Utamaduni na Makumbusho cha Karonga) ni kituo cha kitamaduni na makumbusho katika Wilaya ya Karonga, kaskazini mwa Malawi[1].

Historia hariri

Makumbusho ya Karonga yalifunguliwa rasmi na Rais wa wakati huo Bingu wa Mutharika mnamo Novemba 2004.

Dhamira ya Kituo hiki ni kuhifadhi na kukuza urithi wa asili na kitamaduni wa Karonga. Ugunduzi wa mabaki ya kale ya Dinosaurs na binadamu wa kale na mabaki ya kabla ya historia yaliyoonyeshwa kwenye jumba la makumbusho hutoa maarifa kuhusu asili ya binadamu na historia ya maisha duniani[2][3].

Makusanyo hariri

Ukusanyaji, uhifadhi na uonyeshaji wa vitu vya kale unafanywa na Idara ya Mambo ya Kale, chini ya Idara ya Utamaduni, katika Wizara ya Habari, Utalii na Utamaduni kwa ushirikiano na taasisi ya Uraha. Msisitizo wa kipengele cha Maonyesho ya Utamaduni ni ushirikishwaji wa jamii, viongozi wa kimila na jamii walitakiwa kusaidia katika kukusanya makusanyo mbalimbali kwa ajili ya maonyesho[4].

Jumba la Makumbusho lina maonyesho kuu ambayo yametawaliwa na mabaki ya umri wa miaka milioni 130 ya Malawisaurus, ambavyo yaligunduliwa kilomita 45 kusini kutoka sehemu ya katikati[5].

Marejeo hariri

  1. https://web.archive.org/web/20101203184325/http://www.africom.museum/museums/malawi2.html
  2. "The Cultural & Museum Center Karonga - Fossils"
  3. "CMCK". web.archive.org. 2008-11-19. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-11-19. Iliwekwa mnamo 2022-03-19. 
  4. "Ministry of Information, Tourism, and Culture"
  5. "The Cultural & Museum Center Karonga, Museum"