Karonga ni mji kaskazini mwa Malawi kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa. Ni makao makuu ya Wilaya ya Karonga inayopakana na Tanzania.

Mji Mkongwe, Karonga. Kaskazini mwa Malawi
Mji Mkongwe, Karonga. Kaskazini mwa Malawi

Mnamo mwaka 2018, Karonga ilikadiriwa kuwa na wakazi 61,609.

Jiografia hariri

Karonga iko kwenye mwinuko wa mita 478 juu ya UB kwenye ufuo wa magharibi wa Ziwa Nyasa.[1]

Historia hariri

Zana za zama za mawe za kale na mabaki ya viumbehai waliofanana na binadamu wa kwanza zinaonyesha kwamba maeneo ya Karonga yalikaliwa mapema sana.

Ugunduzi huo ulikuwa katika eneo la uchimbaji wa Malema km 10 (mi 6) kutoka Karonga.

Wakati wa karne ya 19 kabla ya mwaka 1877 Karonga ilifahamika ngome ya Mlozi aliyekuwa mfanyabiashara wa watumwa.[2] Mnamo 1883 kituo cha biashara cha Uingereza kilifunguliwa huko ambacho kiliendelea kikawa chanzo cha mji wa leo. [2] Mvumbuzi Mwingereza Harry Johnston alivamia ngome ya Mlozi na kumaliza utawala wake. [2] Kuanzia hapo Karonga ikawa kituo muhimu cha biashara na kilimo. [2]

Mnamo Desemba 2009 eneo hilo lilipata mfululizo wa matetemeko ya ardhi.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. "Maps, Weather, and Airports for Karonga, Malawi". FallingRain Genomics. Iliwekwa mnamo 21 June 2008.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Karonga". Encyclopædia Britannica. 2008. http://www.britannica.com/EBchecked/topic/312634/Karonga. Retrieved 8 August 2008.