Makumbusho ya Wanawake ya Muso Kunda
Makumbusho ya Wanawake ya Muso Kunda, yaliyoanzishwa mwaka 1995, ni taasisi inayojitolea kuonyesha na kukuza dhamira ya wanawake nchini Mali. Jumba la Makumbusho lilianzishwa na mwanafeministi na mwanahistoria wa Mali Adame Ba Konaré huko Bamako[1]. Jumba la makumbusho linajaribu kuvunja mila potofu ya wanawake, kusherehekea michango yao, kutetea haki zao na kuunda nafasi za mazungumzo.
Kuanzishwa
haririJumba la makumbusho lilianzishwa Bamako mwaka wa 1995[2] na mwanafeministi na mwanahistoria Adame Ba Konaré[3]. Adame ndiye mke wa Rais Alpha Oumar Konaré[3].
Jumba la makumbusho linalenga kukuza na kutetea haki wanawake. Jumba la makumbusho linalenga kukuza ujuzi wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maisha huku likishughulikia masuala ya kitamaduni na ya kisasa[4]. Makumbusho hayo yanatamani kuwa nafasi ambayo inakuza "kumbukumbu" ya wanawake.