Kinengenenge

Ndege wadogo wa familia Zosteropidae
(Elekezwa kutoka Manja)
Kinengenenge
Kinengenenge wa Madagaska
Kinengenenge wa Madagaska
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Zosteropidae (Ndege walio na mnasaba na vinengenenge)
Bonaparte, 1853
Ngazi za chini

Jenasi 14:

Vinengenenge au manja ni ndege wadogo wa familia Zosteropidae. Wana rangi ya zeituni mgongoni na ya kijivu chini na mara nyingi rangi ya manjano na nyeupe pia, pengine nyekundu. Takriban spishi zote zina doa la mviringo kuzunguka macho. Domo lao ni jembamba lenye ncha kali na ulimi ni kama brashi ili kula mbochi. Vinengenenge hula wadudu hasa lakini mbochi na matunda pia. Hulijenga tago lao mtini na jike huyataga mayai buluu 2-4.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri