Manzini (ilikuwa ikijulikana kama Bremersdorp) ni mji mkubwa huko Eswatini (Swaziland), ambao pia ni mji wa Mkoa wa Manzini.

Mji huu ni kitovu cha pili kwa ukubwa nchini, nyuma ya mji mkuu Mbabane, na una idadi ya watu ya 110,000 (2008). Inajulikana kama "Kitovu" cha Eswatini na iko kwenye barabara ya MR3. Eneo kuu la viwanda la Eswatini lililo Matsapha liko karibu na mpaka wa magharibi wa mji huu.

Marejeo

hariri