Mbabane
Mbabane ni mji mkuu wa Eswatini ikiwa na wakazi 70,000 (2003). Ofisi za serikali ziko huko lakini bunge na jumba la mfalme yako mjini Lobamba.
Jiji la Mbabane | |
Nchi | Eswatini |
---|
Mji uko kwenye milima ya Mdimba kwenye kimo cha mita 1200 juu ya UB.
Historia
haririMji ulianzishwa na Waingereza mwaka 1902 BK baada ya vita dhidi ya makaburu ukawa makao makuu ya kiutawala ya eneo la Uswazi.
Jina limetokana na chifu Mbabane Kunene aliyekuwa mkuu wa sehemu ile wakati wa kuunda mji.
Uchumi
haririNguvu ya kiuchumi ya Mbabane ni migodi ya karibu ya bati na dhahabu.
Viungo vya nje
hariri- Maelezo kuhusu Mbabane (Kiing.) Ilihifadhiwa 14 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mbabane kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |