Mark Elliot Zuckerberg (amezaliwa 14 Mei 1984) ni mjasiriamali Mmarekani anayejulikana kama mwanzilishi mwenza wa tovuti maarufu ya urafiki mtandao ya Facebook. Zuckerberg alianzisha Facebook pamoja na wanafunzi wenzake Dustin Moskovitz, Eduardo Saverin, na Chris Hughes wakati wakihudhuria Chuo Kikuu cha Harvard. Zuckerberg ndiye Afisa Mkuu Mtendaji wa Facebook.[2] Amekuwa mada ya utata kuhusu asili ya biashara yake.

Mark Zuckerberg

Mark Zuckerberg in 2011
Amezaliwa Mark Elliot Zuckerberg
14 Mei 1984 (1984-05-14) (umri 40)
White Plains, New York, USA
Kazi yake Co-founder, CEO & President of Facebook
Dini Mkanaji Mungu[1]

Time ilimworodhesha Zuckerberg kama moja wa Watu Mashuhuri Zaidi Duniani mwaka wa 2008. Aliorodheshwa katika kitengo cha Wanasayansi na Mamajuzi kwa mtandao wake ulionoga wa Facebook, na kuorodheshwa wa 52 kati ya watu 101 [3] Kufikia Januari 2010 Zuckerberg ndiye mfanyabiashara aliyejijenga mchanga zaidi mwenye thamani ya zaidi ya dola bilioni. [4]

Maisha ya Awali

hariri

Zuckerberg alizaliwa White Plains, New York na kukulia Dobbs Ferry, New York. Alianza kuunda programu alipokuwa katikati shule ya kitengo cha kati. Zuckerberg alifurahia kuunda programu za kompyuta mapema, na hasa zana za mawasiliano na michezo. Kabla ya kuhudhuria Exeter Phillips Academy, Mark alienda shule ya Ardsley High School. "Katika shule ya upili, yeye alifaulu sana katika masomo ya Kale. Alihamishiwa Phillips Exeter Academy ambako alizama katika somo la Kilatini. [5][5]Pia aliunda programu ya kuwasaidia wafanyakazi katika ofisi ya baba yake kuwasiliana; akaunda toleo la mchezo wa Risk na programu ya kucheza muziki iitwayo Synapse iliyotumia wangafu kujifunza tabia za kusikiliza za watumiaji. Microsoft na AOL zilijaribu kununua Synapse na kumwajiri Zuckerberg, lakini aliamua badala yake kuenda Chuo Kikuu cha Harvard, ambapo alijiunga na Alpha Epsilon Pi , kikundi cha wanafunzi Wayahudi.[6]Chuoni, alijulikana kwa kukariri mistari kutoka mashairi ya kale kama vile The Iliad . [5]

Facebook

hariri
 
Zuckerberg (kulia) na Robert Scoble mwaka 2008.

Uanzilishi

hariri

Zuckerberg alivumbua Facebook katika chumba chake cha kulala cha Harvard mnamo 4 Februari 2004. Wazo la Facebook lilimjia kutoka siku zake za Phillips Academy Exeter ambapo, kama vyuo na shule nyingi, ilikuwa na mazoea ya siku nyingi ya kuchapisha kitabu cha kila mwaka chenye picha za wanafunzi wote, Kitivo na wafanyakazi inayojulikana kama "Facebook". Chuoni, Facebook ilianza tu kama "jambo la Harvard", mpaka Zuckerberg alipoamua kuieneza Facebook katika shule zingine na kuomba msaada kutoka kwa Dustin Moskovitz aliyekuwa wakiishi katika chumba kimoja chuoni. Kwanza walieneza hadi Stanford, Dartmouth, Columbia, Cornell na Yale, na kisha kwa shule nyingine zilizokuwa na mawasiliano ya kijamii na Harvard. [7][8]

Kuhamia California

hariri

Zuckerberg alihamia Palo Alto, California, pamoja na Moskovitz na baadhi ya marafiki zake. Walikodisha chumba kidogo ambacho kilitumika kama ofisi yao ya kwanza. Wakati wa kiangazi, Zuckerberg alikutana na Peter Thiel ambaye imewekeza katika kampuni yake. Walipata ofisi yao ya kwanza wakati wa majira ya kiangazi ya 2004. Kulingana na Zuckerberg, kikundi kilipanga kurudi Harvard kabla ya majira ya baridi lakini hatimaye akaamua kubakia California. Hadi leo, yeye hakuwahi kurudi chuoni kama mwanafunzi.

News Feed

hariri

Mnamo 5 Septemba 2006, Facebook illibua News Feed, huduma ya kuonyesha nini marafiki wako walikuwa wanafanya katika tovuti. Zuckerberg alikashifiwa na baadhi ya watu ‹See Tfd›[weasel words] walioona News Feed kama kitu kisichohitajika na kama chombo cha kunyemelea mtandao.

Facebook Platform

hariri

Mnamo 24 Mei 2007, Zuckerberg ilivumbua Facebook Platform, jukwaa ya maendelezo kwa kujengea vipengele vya kirafiki ndani ya Facebook. Tangazo hili lilisababisha hamu kubwa katika jamii ya wanaotengeneza vipengele hivi. Katika wiki chache, vipengele vingi vilijengwa na baadhi zao tayari kutumika na mamilioni ya watumiaji. Hii leo, kuna zaidi ya watengenezaji 800,000 ulimwenguni wanaounda vipengele kwa kutumia Facebook Platform.

Mnamo 23 Julai 2008, Zuckerberg alitangaza Facebook Connect, toleo la Facebook Platform kwa watumiaji.

Facebook Beacon

hariri

Tarehe 6 Novemba 2007, Zuckerberg ilitangaza mfumo mpya wa matangazo ya kirafiki katika hafla moja mjini Los Angeles. Sehemu ya mpango huu mpya iitwayo Beacon, ingewawezesha watu kushiriki habari na marafiki zao wa Facebook kwa msingi wa shughuli zao katika tovuti nyingine. Muuzaji wa eBay, kwa mfano, angeweza kuruhusu marafiki kujua papo hapo alichokua akiuza kupitia Facebook habari alipokuwa akiorodhesha vitu.

Mpango huu uliibua hoja nzito kuhusu faragha kutoka kwa vikundi na watumiaji binafsi. Zuckerberg na Facebook walishindwa kujibu wasiwasi huu kwa haraka, na mnamo 5 Desemba 2007, Zuckerberg hatimaye aliandika makala katika Facebook na [9] kuchukua jukumu kwa masuala kuhusu Beacon na kutoa njia rahisi kwa watumiaji kujitoa kutoka kwa huduma hiyo.

Utata wa ConnectU

hariri

Wanafunzi wa Harvard Cameron Winklevoss, Tyler Winklevoss, na Divya Narendra walimshtakia Mark kwa kuwahadaa kwa kuwafanya waamini kuwa angeweza kuwasaidia kujenga mtandao wa kijamii ulioitwa HarvardConnection.com (baadaye ulioitwa ConnectU). [10]Walifungua kesi mahakamani mwaka wa 2004 lakini ikafutiliwa mbali bila mapendeleo tarehe 28 Machi 2007. Ilirudishwa mahakamani punde tu baadaye katika Mahakama ya Wilaya ya Marekani huko Boston, na kupangiwa kusikizwa kwa mara ya kwanza mnamo 25 Julai 2007. [11] Katika kusikizwa kwake jaji aliiambia ConnectU kuwa sehemu fulani za malalamiko yao hazikuwa zimekamilika na akawapa fursa ya kufanya marekebisho na kuyawasilisha malalamiko yao tena. Tarehe 25 Juni 2008, kesi iliamuliwa na Facebook kukubalia kuwalipa dola million 65. [12]

Kama sehemu ya daawa hii, mnamo Novemba 2007, nyaraka za siri za mahakamani ziliwasilishwa kwenye tovuti ya gazeti la wanafunzi wa zamani wa Harvard02,138. Zilikuwa ni pamoja na nambari ya usalama wa kijamii ya Zuckerberg, na anwani za wazazi wake na mpenzi wake. Facebook ilienda mahakamani ikitaka hati hizo zitolewe, lakini hakimu ilitoa uamuzi ulioipa 02138 ushindi. [13]

Microsoft kuwekeza katika Facebook

hariri

Mnamo 24 Oktoba 2007, Facebook Inc iliuza asilimia 1.6 ya hisa zake kwa Microsoft Corp kwa dola milioni 240, na kughairi maombi kutoa kwa kampuni inayoongoza katika huduma ya kutafuta katika mtandao Google Inc Hii ilionyesha kwamba Facebook ilikuwa na thamani ya dola bilioni 15 wakati wa mauzo. Programu ya kusasisha bidhaa ya michezo ya Xbox 360 ya Microsoft ilitolewa na pia kuboresha Facebook, Twitter na Last.fm [14]

Facebook mwaka wa 2009

hariri

Kufikia 2 Desemba 2009 Facebook ilidai kuwa ina watumiaji wasiopungua milioni 350.

Filamu

hariri

Kuna sinema kuhusu Mark Zuckerberg na waumbaji wa Facebook, iitwayo The Social Network . Inapaswa kutolewa mwaka wa 2010, na ina waigizaji nyota Jesse Eisenberg na Justin Timberlake.

Bibliografia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Vara, Vauhini (2007-11-28). "Too Much Information? - WSJ.com". Online.wsj.com. Iliwekwa mnamo 2009-08-21.
  2. Reagan, Gillian (2009-03-10). Thumbs Up! There's a Lot to Like about 'Like' (HTML). The New York Observer. The New York Observer, LLC. Retrieved on 2009/03/11
  3. Time Magazine Ilihifadhiwa 10 Machi 2010 kwenye Wayback Machine. 100 Watu 100 Mashuhuri Zaidi
  4. Forbes Asia Asia's Youngest Self-Made Billionaire
  5. 5.0 5.1 5.2 McDevitt, Caitlin. "What We Learned About Mark Zuckerberg This Week", The Big Money, 2010-03-05. Retrieved on 2010-03-05. Archived from the original on 2010-03-08.  Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "whatwelearned" defined multiple times with different content
  6. "Hacker. Dropout. CEO".
  7. https://web.archive.org/web/20070105155512/http://daily.stanford.edu/article/2004/3/10/thefacebookcomsDarkerSide = clnk & cd = 2 & gl = ca & client = firefox-a
  8. "Online network created by Harvard students flourishes". Tufts Daily. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-29. Iliwekwa mnamo 2009-08-21.
  9. The Facebook Blog | Facebook
  10. Nicholas Carlson. "In 2004, Mark Zuckerberg Broke Into A Facebook User's Private Email Account". Silicon Alley Insider. Iliwekwa mnamo 2010-03-05.
  11. "PC World - Facebook Tries to Fend Off Copyright-Infringement Claim". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-30. Iliwekwa mnamo 2010-03-19.
  12. Logged in as click here to log out. "Facebook paid up to $65m to founder Mark Zuckerberg's ex-classmates | Technology | guardian.co.uk". Guardian. Iliwekwa mnamo 2009-08-21.
  13. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named autogenerated1
  14. "Microsoft investes $ 240 milioni in Facebook - MSNBC.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-04-17. Iliwekwa mnamo 2010-03-19.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: