Microsoft
Microsoft Corporation ni kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya kompyuta. [2] Neno Microsoft ni neno unganifu lilitokana na maneno ya Kiingereza "microcomputer" na "software".
Ilipoanzishwa | Albuquerque, New Mexico (Aprili 4, 1975 )[1] |
---|---|
Makao Makuu | Redmond, Washington, Marekani |
Mapato kabla ya riba na kodi | US$ 20.363 billion (2009) |
Net income | US$ 14.569 billion (2009) |
Total equity | US$ 39.558 billion (2009) |
Tovuti | djt5 www.microsoft.com |
Kampuni ilianzishwa na William Henry Gates III (anayefahamika zaidi kama Bill Gates) na Paul Allen 04 Aprili 1977, ili kuendeleza na kuuza mifumo-ongozo rahisi kwa ajili ya kompyuta ndogo za Altair 8800. Kampuni hili liliinuka na kutawala soko la utengenezaji wa mifumo-ongozo ya kompyuta binafsi kupitia mfumo wake unaojulikana kama MS-DOS (Microsoft - Disk Operating System) katikati ya miaka ya 1980, ikifuatiwa na programu ya Microsoft Windows[3].
Makao makuu yako Redmond, Washington, Marekani.
Kampuni hii inaendeleza, kutengeneza, kutoa leseni, kusaidia na kuuza programu za kompyuta, vifaa vya umeme, kompyuta binafsi pamoja na huduma zihusianazo na hizo. Programu yake ya kompyuta ijulikanayo sana ni mfumo ongozo wa kompyuta wa Microsoft Windows, na programu nyingine kama vile, Microsoft Office, na Internet Explorer pamoja na Edge Web. Vifaa vyake maarufu ni vifaa michezo vya Xbox pamoja na mfumo wa kioomguso uitwao Microsoft Surface lineup kwa ajili ya kompyuta binafsi.
Kwa mwaka wa 2016, ndiyo kampuni kubwa duniani yenye kutengeneza programu za kompyuta kwa makusanyo ya jumla, na ni moja kati ya kampuni zenye thamani kubwa zaidi duniani. Microsoft ni kampuni iliyoko nafasi ya 31 katika orodha ya mwaka 2018 ya Fortune 500 ya mashirika makuu makubwa ya Marekani na mapato ya jumla.
Historia
haririMicrosoft ni kampuni kubwa ya teknolojia ya habari iliyoanzishwa mnamo tarehe 4 Aprili mwaka 1975, na Bill Gates na Paul Allen huko Albuquerque, New Mexico, Marekani. Kampuni hii ilianza kama kampuni ya kuuza lugha ya programu ya msimbo kwa kompyuta, lakini haraka ikawa mmoja wa watengenezaji wakubwa wa programu za kompyuta ulimwenguni.
Historia ya Microsoft imejaa mafanikio na uvumbuzi wa teknolojia. Mwaka 1985, kampuni hiyo ilizindua Windows 1.0, mfumo wa uendeshaji wa kompyuta uliofanikiwa kwa soko kwa kutumia mwonekano wa picha. Tangu wakati huo, Microsoft imekuwa ikitoa matoleo mengi ya Windows pamoja na bidhaa nyingine kama vile Microsoft Office Suite, Internet Explorer, na Xbox.
Katika miaka ya 1990 na 2000, Microsoft ilikuwa kiongozi katika soko la programu ya kompyuta na inasemekana kuwa mojawapo ya kampuni za teknolojia tajiri zaidi ulimwenguni. Walakini, kampuni hiyo imekabiliwa na changamoto kadhaa za kisheria na ushindani wa soko katika miaka ya hivi karibuni.
Leo, Microsoft bado ni mojawapo ya makampuni ya teknolojia yenye ushawishi mkubwa ulimwenguni, ikitoa suluhisho za programu na vifaa vya kompyuta kwa watumiaji binafsi na wafanyabiashara.
Tanbihi
hariri- ↑ "Bill Gates: A timeline". news.bbc.co.uk. BBC News. 2006-06-15. Iliwekwa mnamo 2008-08-18.
- ↑ "Microsoft Corporation Annual Report 2005" (doc). Microsoft. Iliwekwa mnamo 2005-10-01.
- ↑ "Information for Students: Key Events In Microsoft History" (doc). Microsoft Visitor Center Student Information. Iliwekwa mnamo 1 Oktoba 2005.
Viungo vya nje
hariri- Microsoft - tovuti rasmi
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Microsoft kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |