Mary Mgonja
Mary Mgonja ni mwanasayansi wa kilimo kutoka Tanzania na mzalishaji wa mimea, pia ni mkurugenzi wa teknolojia na mawasiliano katika kampuni ya kilimo ya Namburi ya nchini Tanzania.
Mary Mgonja | |
Amezaliwa | Tanzania |
---|---|
Kazi yake | mwanasayansi wa kilimo, mkurugenzi wa teknolojia |
Elimu
haririMary Mgonja ana shahada ya uzamivu katika falsafa na uzalishaji wa mimea. Shahada hiyo ameipata katika chuo cha Ibadani na International Institute of Tropical Agriculture.
Uzoefu wa kazi
haririMgonja amefanya kazi kama mwansayansi mkuu katika kuboresha kilimo cha ukame katika Taasisi ya Mazao sehemu zenye ukame katika maeneo ya Patancheru Hyderabad,Telangana nchini India.
Anaiwakilisha Tanzania katika Southern African Development Community (SADC) na East African Community (EAC). Pia amefanya kazi kama mkurugenzi wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) ambayo ni shirika linalosaidiwa na Bill and Melinda Foundation na Rockerfeller Foundation.[1]
Marejeo
hariri- ↑ The Citizen Correspondent (8 Agosti 2016). "Body wants agriculture to go hi-tech". The Citizen. Dar es Salaam. Iliwekwa mnamo 22 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mary Mgonja kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |