Gundi (mnyama)

(Elekezwa kutoka Massoutiera)
Gundi
Gundi kaskazi (Ctenodactylus gundi)
Gundi kaskazi (Ctenodactylus gundi)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia
Nusuoda: Hystricomorpha
Familia: Ctenodactylidae
Gervais, 1853
Ngazi za chini

Jenasi 4, spishi 5:

Gundi (kutoka Kiingereza: gundi) au panya-kichanuo (kutoka Kiingereza: comb rat) ni wagugunaji wadogo wa familia Ctenodactylidae wanaotokea kaskazini kwa Afrika. Huishi katika majangwa yenye miwamba. Mwili wao ni mnono wenye urefu wa sm 17-18 na unafunikwa kwa manyoya laini. Wana miguu mifupi, macho makubwa na mkia mfupi. Miguu yote ina vidole vinne tu na vile vya kati vya miguu ya nyuma vina nywele ngumu zinazofananana na kichanuo (sababu ya jina la panya-kichanuo). Hula kila aina ya mmea ipatikanayo, lakini, kama wanyama wengi wa jangwa, hawakunywi na hupata maji yote wanayoyahitaji kutoka chakula chao[1]. Jike huzaa watoto wawili kila mara baada muda wa mimba wa mieze miwili. Kwa sababu ya uhitaji wa kuhifadhi maji jike hutoa maziwa machache tu na watoto hulikizwa kabisa baada ya wiki nne.

Gundi huishi katika makoloni ya wanyama hadi mia moja au zaidi, lakini idadi ni ndogo katika maeneo ambapo chakula ni adimu. Hawatengenezi matundu ya aushi lakini hujisitiri katika mianya ya miamba usiku au mchana wakati wa joto kubwa. Wanyama hawa hufanya sauti sana na wana namba ya sauti za alamu na mawasiliano ambazo zinawasaidia kwa kugundisha makundi yao.

Spishi hariri

Picha hariri

Marejeo hariri

  1. Macdonald (Ed), Professor David W. (2006). The Encyclopedia of Mammals. Oxford University Press. ISBN 0-19-920608-2. 
  Makala hii kuhusu "Gundi (mnyama)" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili gundi, comb rat kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni gundi, panya-kichanuo.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.