John Edward Gray (2 Februari 18007 Machi 1875) alikuwa mtaalamu Mwingereza wa zoolojia wakati wa karne ya 19.

John Edward Gray

Alizaliwa mtoto wa baba mfarmasia aliyekusanya mimea. Mwenyewe alisoma tiba mjini London na mwaka 1824 aliajiriwa na idara ya zoolojia kwenye Makumbusho ya Kibritania. Akaendelea kuwa mkurugenzi wa idara hii tangu 1840 akaiongoza hadi 1874.

Wakati wake ilikuwa kipindi cha uenezaji wa Milki ya Britania kote duniani na hii ilimsaidia kuongeza sana sampuli za wanyama wa kila aina kutoka pande zote za dunia. Chini ya uongozi wake mkunsanyiko wa kisayansi wa sampuli za wanyama uliendelea kuwa bora duniani.

Kazi hii ilimleta kuainisha mamia ya spishi za wanyama na ndege na kwa hiyo jina lake linakumbukwa katika majina ya spishi alizotangulia kueleza kisayansi.

Alipenda pia stempu za posta alikuwa kati ya watu wa kwanza duniani waliokusanya stempu.

Mdogo wake George Robert Gray alimfuata kaka akaongoza idara ya ndege kwenye makumbusho na kuwa maarufu pia katika uainishaji wa ndege na vipepeo hasa.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John Edward Gray kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.