Maurice Michael Otunga

Maurice Michael Otunga (Januari 1923 - 6 Septemba 2003) alikuwa askofu wa kanisa katoliki na kardinali wa kwanza nchini Kenya.

Otunga alizaliwa mwaka 1923 kwenye kijiji cha Chebukwa katika wilaya ya Bungoma. Babake alikuwa chifu wa koo la Bakhone katika kabila Wabukusu mwenye wake 40.

Maurice alibatizwa kwa umri wa miaka 12 akamaliza masomo yake ya shule Mangu High School. Baadaye akajiunga na seminari ya Kakamega akaendelea masomo ya upadre kwenye semianri ya Gaba (Kampala - Uganda). Masomio ya juu akafuata huko Roma kwenye chuo kikuu cha Papa alipopadrishwa mwaka 1950 pamoja na kupokea cheo cha daktari.

Baada ya kurudi Kenya akawa mwalimu kwenye seminari ya Kisumu hadi 1956 alipoteuliwa kuwa askofu msaidizi wa Kisumu.

1960 alikabidhiwa dayosisi mpya ya Kisii kama askofu wake wa kwanza. 1969 akawa msaidizi wa askofu kuu wa Nairobi na 1971 alikuwa askofu mkuu wa kwanza Mwafrika.

Tar. 5 Machi 1973 Papa Paulo VI akampa cheo cha kardinali.

Otunga akajiuzulu 1997 alipofikia umri wa miaka 75 akachagua nyumba ya wazee maskini kama makao yake ya uzeeni.

Kardinali Maurice Michael Otunga aliaga dunia 6 Septemba 2003 akiwa na umri wa miaka 80.

Mwaka 2005 kulitokea fitina juu ya kaburi lake kati ya kanisa katoliki na jumuiya ya Wabukusu. Askofu Mkuu Mwana a'Nzeki alimua kuhamisha maiti ya kardinali kutoka makaburi ya mjini kwenda Resurrection Gardens na kumzika katika kanisa dogo huko wakati kanisa la Kenya lafuatilia shughuli za kumtangaza marehemu kuwa mwenye heri. Wasemaji wa Wabukusu walipinga mipango hii kwa hofu ya kwamba tendo litaleta balaa juu ya kabila.

Viungo vya Nje

hariri