Bungoma ni mji wa Kenya ya magharibi karibu na mpaka wa Uganda ambao ni makao makuu ya kaunti ya Bungoma.

Bungoma
Bungoma

Lua error in Module:Location_map at line 510: Unable to find the specified location map definition: "Module:Location map/data/Kenya" does not exist.Mahali pa mji wa Bungoma katika Kenya

Majiranukta: 0°34′0″N 34°34′0″E / 0.56667°N 34.56667°E / 0.56667; 34.56667
Nchi Kenya
Kaunti Bungoma
Idadi ya wakazi
 - 81,151

Wakazi walikuwa 81,151 wakati wa sensa ya mwaka 2009[1].

Bungoma iko kwenye kimo cha mita 1,385 juu ya UB, mguuni pa Mlima Elgon.

Wenyeji wa Bungoma ni Wabukusu ambao ni tawi la Waluhya.

Mji wa Bungoma ulianzishwa kama kituo cha reli ya Uganda katika miaka ya 1920. Bungoma ikateuliwa kama kituo cha mwisho ndani ya Kenya kabla ya kufikia mpaka wa Uganda.

Wakati wa uhuru Bungoma ilionekana kama kijiji kikubwa chenye maduka machache. Mji ukaendelea kukua haraka.

Uchumi umetegemea hasa kilimo kinachostawi vizuri kutokana na hali ya hewa na wingi wa mvua. Kuna kiwanda cha sukari. Kiwanda cha karatasi cha Webuye kipo karibu.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  1. Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.