Maurice Omondi Odumbe (amezaliwa mnamo 15 Juni 1969) alikuwa mchezaji wa kriketi mwenye uraia wa Kikenya ambaye alipigwa marufuku kutoshiriki katika mchezo wa kriketi mnamo Agosti 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kupokea fedha kutoka kwa watu wasiohalali.

Maurice Odumbe
Personal information
Full name Maurice Omondi Odumbe
Batting style Mkono wa kulia
Bowling style Mkono wa kulia offbreak
Role Batsman
International information
National side Kenya
ODI debut (cap 7) 18 Februari 1996 v Uhindi
Last ODI 8 April 2003 v Pakistan
Domestic team information
Years Team
1995/96–2003/04 Kenya
Career statistics
Competition ODI FC LA
Matches 61 17 102
Runs scored 1,409 893 2,363
Batting average 26.09 34.34 26.85
100s/50s 0/11 3/3 1/14
Top score 83 207 119
Balls bowled 2,237 2,016 3,968
Wickets 39 40 88
Bowling average 46.33 19.55 33.88
5 wickets in innings 0 4 1
10 wickets in match 0 1 0
Best bowling 4/38 6/64 5/38
Catches/stumpings 12/0 14/0 34/0
Source: Cricinfo, 8 Mei 2017

Maisha hariri

Alizaliwa katika mji mkuu wa Nairobi na alihudhuria Shule ya Msingi ya Dr. Aggrey na shule ya sekondari ya Upper Hill, ambapo mchezaji huyu ambaye ni “batsman” wa mkono wa kulia na “bowler” wa mkono wa kulia alionyesha hamu na uwezo wa kucheza mchezo wa kriketi. Odumbe alicheza mechi yake ya kwanza kwa timu ya kitaifa ya Kenya mnamo 4 Juni 1990 dhidi Bangladesh katika sehemu ya Amstelveen katika nyara ya ICC, alifunga 41 na kuchukua 1 / 26 na alikuwa amekuwa mmoja wa wachezaji wao wanaoongoza wa One Day International (ODI) katika mechi yake ya kwanza ya kombe la dunia la Kriketi mwaka wa 1996. Odumbe alishinda tuzo la mchezaji bora wa mechi katika mojawapo wa mishtuko kubwa katika mchezo wa kriketi, kwa kuchukua 3 kwa 14 katika ushindi wa Kenya dhidi ya West Indies.

Odumbe alicheza mechi yake ya kwanza ya darasa la kwanza mwaka wa 1998 wakati Kenya ilicheza dhidi ya upande wa A waUingereza uliyokuwa unazuru, alitengeneza 16 na kuchukua 0 / 29, na kuendelea kuichezea vyema upande wake wa mtaa wa Nairobi, klabu ya Aga Khan. Odumbe aliteuliwa nahodha wa kitaifa kabla ya kombe la dunia la kriketi la mwaka wa 1999, na kushinda tuzo la mchezaji bora wa mechi dhidi ya Sri Lanka kwa nje(off) zake 82 kupeana (deliveries) 95. Alipitisha unahodha kwa Steve Tikolo kwa ajili ya kombe la dunia la kriketi la mwaka wa 2003. Odumbe alicheza vizuri kwani Kenya ilifika nusu fainali, na katika mwaka uliyofuata alifikisha alama 207 dhidi ya visiwa vya Leeward, hii ilikuwa alama bora zaid katika wasifu wake.

Mnamoi Machi mwaka wa 2004, Odumbe alichunguzwa na Baraza la Kriketi la Kimataifa (International Cricket Council) kufuatia madai ya “match-fixing” na alipatwa na hatia mnamo Agosti mwaka wa 2004 ya kupokea fedha kutoka watu wasiohalali na kupigwa marufuku kutoshiriki kwa mechi zozote za kriketi kwa muda wa miaka mitano. Huku wachambuzi wakati huo wakiamini kwamba marufuku hii ingesababisha mwisho wa wasifu wake wa kriketi, Odumbe alisema kwamba anapanga kurejea katika mchezo wa kriketi mara tu marufuku hiyo itakapoisha. . Odumbe mechi 61 za ODI, na kufunga mikimbilio 1409 katika 26.09 na kuchukua wiketi 39 katika 46.33 na mechi 17 za daraja ya kwanza (first-class), kufunga mikimbilio 894 katika 34.34 na kuchukua wiketi 40 katika 19.55.

Tangu kupigwa kwake marufuku, Odumbe amekuwa akishiriki kikamilifu katika kutafuta fedha kwa ajili ya malazi kwa yatima wa UKIMWI, na vile vile kuwasilisha programu ya michezo ya redio kila wiki na kuonekana katika idadi ya vitambulisho vya runinga. Pia anapanga kutoa wimbo na ametangaza nia yake ya kusimama kama mgombea wa Umoja wa Maendeleo ya Kidemokrasia ya Kitaifa katika uchaguzi mkuu wa Kenya ujao.

Alirejea kriketi ya ushindani katika kiwango cha mtaa mnamo Agosti 2009, akiwa na umri wa miaka 40

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Filgga, K. (2007) "Rebranded Odumbe Now Playing Different Ball game", The Nation, Nairobi, 17 Machi 2007.
  • Williamson, M. (2004) "Maurice Odumbe", Cricinfo, [1] Accessed 7 Aprili 2007.