Sri Lanka (pia Sirilanka, kwa Kisinhala Śrī Laṃkāva, kwa Kitamil Ilaṅkai; hadi mwaka 1972: Ceylon) ni nchi ya kisiwani katika Asia ya Kusini.

Sri Lanka
Ramani ya Sri Lanka.

Iko karibu na ncha ya kusini ya rasi ya Uhindi katika Bahari Hindi.

Nchi imekaliwa na watu walau kuanzia miaka ya 125,000 KK na ilizidi kupata umuhimu kutokana na mahali ilipo.

Mji mkuu ni Sri Jayawardenapura.

Mikoa hariri

Sri Lanka ina mikoa 9:

Mikoa hiyo imegawanyika katika wilaya 25.

 
Hekalu la Kihindu mjini Colombo.

Watu hariri

Idadi ya wakazi ni takriban milioni 22 (2020).

Walio wengi (74.9%) ni Wasinhala ambao kwa kawaida ni wafuasi wa Ubuddha wa madhehebu ya Theravada (70.2%). Takriban 11.2% ni Watamili ambao wengi wao ni Wahindu (12.6%) na wanaishi hasa kaskazini mwa kisiwa.

Lugha zao, Kisnhala na Kitamil ni lugha rasmi. Pia Kiingereza kinatambulika.

Kuna Wamori Waislamu (9.7%, hasa Wasuni) ambao wengi wao wanajiona machotara wa Kiarabu.

Pia kuna Wakristo (7.4%, hasa Wakatoliki 5.8%, halafu Waanglikana na Waprotestanti wengine) ambao vilevile baadhi yao ni machotara wa Kizungu (hasa wa Kireno na wa Kiholanzi).

Karibu wananchi wote wanajali sana dini katika maisha yao.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Historia
Ramani
Biashara
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sri Lanka kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.