Mnururisho sumakuumeme

(Elekezwa kutoka Mawimbi ya sumakuumeme)

Mnururisho sumakuumeme (ing. electromagnetic radiation / electromagnetic waves) ni mnururisho wa mawimbi zinazounganisha uga sumaku na uga wa umeme na kubeba nishati. Mifano ya mawimbi sumakuumeme ni wimbiredio, mikrowevu, mawimbi ya joto, mawimbi ya urujuanimno, eksirei, na nuru inayoonekana kwetu.

Spektra ya mawimbi sumakuumeme; nuru ni sehemu ya wawimbi haya

Tofauti na mawimbi ya mata kama wimbisauti zile za sumakumeme hazihitaji midia kwa uenezi wao. Zinaenea pia katika ombwe kwa kasi ya nuru.

Mawimbi yenye masafa (wavelength) mafupi ni mnururisho wa kuioniza na hivyo hatari kwa viumbehai kuanzia kiwango fulani, hasa gammarei na eksirei. Hata mnururisho wa urujuanimno ina hatari unaweza kusababisha mbabuko wa jua (ing. sunburn) kwenye ngozi ha hata kansa.

Pande mbalimbali za spektra ya sumakuumeme zinatofautiana kwa masafa ya mawimbi (wavelenghth), marudio (frequency) na kiwango cha nishati zinazosafirisha.