Masafa ya mawimbi
Masafa ya mawimbi (pia urefu wa wimbi[1], mara chache lukoka[2]; kwa Kiingereza wavelength) ni namna ya kupima na kutaja ukubwa wa wimbi.
Ni umbali kati ya sehemu za kulingana za mawimbi mawili ambayo yanafuatana, kwa mfano kati ya kilele na kilele au mabonde yao.
Mawimbi yapo kila sehemu ya mazingira asilia, kwa mfano:
- mawimbi ya maji
- mawimbisauti
- mawimbi sumakuumeme pamoja na nuru na wimbiredio
Masafa ya mawimbi hutofautiana sana. Mawimbi marefu yanayoweza kutambuliwa na milango ya fahamu ya binadamu ni sauti ya besi yenye masafa ya mita 21. Sikio letu linatambua mawimbi yenye masafa kati ya milimita 17 hadi mita 21.
Mawimbi sumakuumeme yana upeo mkubwa.
- Masafa ya wimbiredio ni kati ya milimita 1 hadi kilomita 100.
- nuru inayoonekana kwa macho yetu ina masafa kati ya nanomita 380 (urujuani) hadi 780 (nyekundu). Nyuki huona pia mnururisho mfupi zaidi yaani urujuanimno, lakini hawaoni nyekundu.
- eksirei zina masafa baina ya nanomita 0.01 hadi 10.
- masafa ya mawimbi gammarei iko katika upeo wa pikomita.
Masafa ya mawimbi na marudio
haririMasafa ya mawimbi huwa na uhusiano wa kinyume na marudio ya wimbi. Kama marudio ya wimbi ni ya juu, masafa yake yatakuwa madogo. Vilevile kinyume, kama wimbi lina masafa makubwa, marudio yake ni madogo.
Marejeo
haririTovuti za Nje
hariri- Conversion: Wavelength to Frequency and vice versa – Sound waves and radio waves Archived 11 Machi 2012 at the Wayback Machine.
- Teaching resource for 14–16 years on sound including wavelength Archived 13 Machi 2012 at the Wayback Machine.
- The visible electromagnetic spectrum displayed in web colors with according wavelengths