Mbale ni mji wa Uganda ya kusini-mashariki mwenye wakazi 76,000 kwenye mguu wa mlima Elgon. Ni makao makuu ya wilaya ya Mbale. Umbali na Jinja ni 120 km na 190 km na Kampala.

Mahali pa Mbale katika Uganda.

UchumiEdit

Mazingira ya Mbale kuna kahawa nyingi na pia kilimo cha mazao mengine. Hivyo uchumi wa mji umetegemea kilimo na biashara ya mazao. Kuna pia kiwanda cha maziwa.

UtamaduniEdit

Eneo la Mbale ni nyumbani kwa Wagishu hasa. Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Uganda kipo mjini.

Picha kadhaa za filamu "Casino Royale" zilipigwa Mbale.