Mbale, Kenya
Mbale ni mji wa Kenya katika Kaunti ya Vihiga, moja kati ya kaunti 43 nchini Kenya. Ni makao makuu yake. Huitwa pia Maragoli ambalo ni jina la wenyeji wa eneo hili. Hapa ndipo Sherehe za Kitamaduni za Wamaragoli hufanyikia kila mwaka tarehe 26 Desemba.
Mbale | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Vihiga |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 17,404 |
Kuna mji nchini Uganda ulio na jina sawa.
Mbale una jumla ya wakaazi kutoka makabila tofautitofauti na ni pamoja na Wakikuyu, Wakisii, Wajaluo na makabila mengine ya Waluhya ambayo wenyeji wa mji huo, Wamaragoli, ni baadhi yao. Mji wa bale hoteli kuu 5 na baa kuu 4 ambazo huwahudumia watu kutoka maeneo ya Kisumu, Kakamega na mazingira yake.
Mji wa Mbale pia ni makao makuu ya Wilaya ya Vihiga inajivunia kwa kuwa na makao makuu ya kisasa zaidi kwa wafanyikazi wake wa serikali na polisi wa utawala ambayo yaamejengwa kwa muundo wa majumba yakukodisha ya kisasa. Mji wa Mbale una benki 3 kuu na benki ya Mashirika moja, benki ya Barclays , benki ya Equity na benko ya Kenya Commercial Bank(KCB) na benki ya Mashrika ikiwa Kakamega Teachers Sacco Society ambayo bado haijazinduliwa rasmi lakini inafanya kazi kwa sasa. Mji wa Mbale una zaidi ya wafanyi biashara mia moja na aina za biashara kwa mfano, maduka, ushonaji,usambazaji wa mikate, maduka ya shughuli za tovuti, mahoteli n.k.
Shule
haririMji huu una zaidi ya shule za msingi kumi na shule za sekondari tano - shule kuu zikiwemo Shule ya Msingi ya Hambale , Shalom Academy, Shule ya Msingi ya Mukuli ,Shule ya Sekondari ya Mbale, Shule ya Sekondari ya Kegoye Shule ya Sekondari ya Mbihi.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mbale, Kenya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |