Mchezo wa ng'ombe ni desturi inayojulikana hasa katika nchi za Hispania na Ureno, pia katika maeneo ya jirani ya Ufaransa kusini na katika koloni za zamani za Hispania huko Amerika ya Kilatini kama Meksiko. Imekuwa pia mila ya pekee kwenye Kisiwa cha Pemba, Tanzania. Kila mahali ni mashindano kati ya wanadamu na fahali wa ng'ombe lakini kuna taratibu tofautitofauti.

Torero akimkasirisha ng'ombe dume kwa kitambaa chekundu
Matador akilenga kumwua ngombe kwa upanga wake.

Mchezo wa ng'ombe katika Hispania

hariri

Katika mchezo wa Hispania fahali anauawa uwanjani. Mchezo unafanywa katika uwanja wa pekee unaoitwa Plaza de Toros. Wale wanoshindana na ng'ombe dume wanaitwa "torero"; mkuu wao atakayemwua kwa pigo la upanga wake ni "matador". Matador anatangulia kucheza na fahali kwa kumkasirisha kwa kitambaa chekundu na kutoroka akishambuliwa. Wasaidizi wake wanapita kwa farasi na kumdunga fahali kwa mikuki midogo kwa kusudi la kumdhoofisha. Mwishoni ng'ombe anauawa na matador kwa upanga. Muda wa mchezo ni kama dakika 20 kwa kila mnyama.

Ilhali Wahispania wanaua ng'ombe wa dume Aareno wanawachezea tu hadi kuwaangusha chini bila kuwaua.

Asili za Roma ya Kale

hariri

Historia ya desturi hii inarudi nyuma hadi zamani za Dola la Roma watu walipopenda kuwa na maonyesho ya mapambano ya wanyama pori, ama ya wenyewe kwa wenyewe au zaidi ya watu dhidi ya wanyama hawa. Maonyesho haya yalifanyika katika uwanja wa mji kwa mfano uwanja wa Koloseo huko Roma. Desturi hii imepotea kila sehemu ya eneo la kale la Dola la Roma kwa sababu ilipingwa na kanisa la kikristo isipokuwa Hispania na Ureno.

Mchezo wa ng'ombe Pemba kisiwani

hariri

Pemba ndipo mahali pa pekee katika Afrika penye desturi hii ya mchezo wa ng'ombe. Hii ni kutokana na athira ya Ureno kwenye mwambao wa Afrika ya Mashariki miaka 400 iliyopita. Mara Wareno walikuwa na kituo huko Chake Chake, mara walikuwa na mapatano ya usaidizi na Pemba, mara waliuachia utawala Sultani wa Mombasa. Haijulikani jinsi walivyoacha desturi hii Pemba.

Kuhusu mchezo huu amesema Abdullah Amur Suleiman (http://groups.msn.com/SitiBintiSaad/mchezowangombebullfight.msnw Archived 21 Septemba 2005 at the Wayback Machine.):

Mchezo wa ng’ombe ni mchezo wa taifa huko Pemba, hapana mtoto wa kiume hata mmoja wa Kipemba, akiwa mwenye asili ya Kiafrika au Kiarabu ambaye hajuwi kumcheza Ng’ombe.

Mchezo huu jinsi unavyopendwa na vijana wa kiume wa Pemba ni kama vile wavulana wanavyoupenda mchezo wa mpira yaani ‘football’, huko Zanzibar, Tanzania bara na kwingineko ulimwenguni.

Aghlabu mchezo wa ng’ombe huchezwa wakati wa watu ambao wamerejea mavunoni na karafuu zimekwisha tena na hapo hutazamiya kustarehe. Watu wengi hujumuika kwenye sherehe hizo za mchezo wa ng’ombe na hawaji tu kuona mchezo huo lakini hulipa ada maalum kwa ajili ya kuuona namna mchezo huo ufanywavyo na mastadi wake hodari.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Mchezo wa ng'ombe kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.