Desturi (kutoka Kiarabu) ni jambo lá kawaida linalotendwa na jamii fulani mara kwa mara. Neno hilo ni sawa na mazoea, ada au kaida.

Kawaida au desturi ya watoto kupata mulo wao wawapo kwenye kuchunga mifugo ya ng'ombe au mbuzi

Kwa kawaida kila jamii huwa na desturi zake. Pia desturi huweza kutokea kwa mtu binafsi. Imezoeleka katika jamii zetu, desturi huambatana na mila. Ukichunguza kwa undani katika jamii nyingi za Afrika, mila ndiyo hujenga desturi ingawa wengi wetu tunashindwa kutofautisha dhana ya neno 'mila' na neno 'desturi'.

Mfano wa desturi ni adabu na utaratibu wakati wa kula. Hapa utabaini kwamba, kila kabila lina mazoea yake ya kuliendea jambo hilo.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Desturi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.