Mdudu-kijiti
Mdudu-kijiti (Achrioptera fallax)
Mdudu-kijiti (Achrioptera fallax)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Linnaeus, 1758
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Lang, 1888
Oda: Phasmatodea
Jacobson & Bianchi, 1902
Ngazi za chini

Nusuoda 3:

Wadudu-kijiti au vijiti vitembeavyo ni wadudu warefu wa oda Phasmatodea (phasma = kizuka) ambao wanafanana na vijiti. Wadudu-jani au majani matembeayo wa familia Phylliidae ni wanachama wa oda hii pia.

Wadudu hawa ni wembamba na warefu isipokuwa spishi za Phylliidae ambazo ni pana. Spishi kadhaa ni wadudu warefu kabisa katika dunia. Jike la Phobaeticus chani ni mrefu kuliko wote wengine na ana urefu wa sm 36 (57 kama miguu ikinyumbulika). Muundo wa mwili ni kamafleji na unafanana na kijiti au jani. Spishi nyingi hazina mabawa au zina mabawa yaliyopunguka. Mabawa ya mbele ni membamba na magumu lakini yale ya nyuma ni mapana yakiwa yamekunjuka.

Jenasi za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Bactricia
  • Bactrododema
  • Burria
  • Clonaria
  • Hemipachymorpha
  • Leptynia
  • Mantis
  • Maransis
  • Pachymorpha
  • Phthoa
  • Tuberculatocharax
  • Ulugurucharax
  • Xylica
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu-kijiti kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu "Mdudu-kijiti" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili stick insect, walking stick, leaf insect na walking leaf kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni mdudu-kijiti, kijiti kitembeacho, mdudu-jani na jani litembealo.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.