Mdudu-kijiti
(Elekezwa kutoka Phasmatodea)
Mdudu-kijiti | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mdudu-kijiti (Achrioptera fallax)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Nusuoda 3: |
Wadudu-kijiti au vijiti vitembeavyo ni wadudu warefu wa oda Phasmatodea (phasma = kizuka) ambao wanafanana na vijiti. Wadudu-jani au majani matembeayo wa familia Phylliidae ni wanachama wa oda hii pia.
Wadudu hawa ni wembamba na warefu isipokuwa spishi za Phylliidae ambazo ni pana. Spishi kadhaa ni wadudu warefu kabisa katika dunia. Jike la Phobaeticus chani ni mrefu kuliko wote wengine na ana urefu wa sm 36 (57 kama miguu ikinyumbulika). Muundo wa mwili ni kamafleji na unafanana na kijiti au jani. Spishi nyingi hazina mabawa au zina mabawa yaliyopunguka. Mabawa ya mbele ni membamba na magumu lakini yale ya nyuma ni mapana yakiwa yamekunjuka.
Jenasi za Afrika ya Mashariki
hariri- Bactricia
- Bactrododema
- Burria
- Clonaria
- Hemipachymorpha
- Leptynia
- Mantis
- Maransis
- Pachymorpha
- Phthoa
- Tuberculatocharax
- Ulugurucharax
- Xylica
Picha
hariri-
Agathemerodea/Agathemeridae (Agathemera crassa)
-
Timematodea/Timematidae (Timema sp.)
-
Verophasmatodea/Diapheromeridae (Bactrododema tiaratum)
-
Verophasmatodea/Phylliidae (Phyllium jacobsoni)
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu-kijiti kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |