Mdudu Mabawa-potwa

Mdudu mabawa-potwa
Stylops melittae
Stylops melittae
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Strepsiptera (Wadudu wenye mabawa yaliyopotwa)
Kirby, 1813
Ngazi za chini

Nusuoda 2 na familia 12

Wadudu mabawa-potwa ni wadudu wadogo wa oda Strepsiptera (strepsis = iliyopotwa, ptera = mabawa) wenye mabawa yaliyopotwa. Wadudu hawa ni wadusia wa wadudu wengine, kama nyuki, nyigu, sisimizi, warukaji-majani, mende, panzi na visamaki-fedha.

Madume ya wadudu hawa wana mabawa, miguu, macho na vipapasio kama wadudu wengine, lakini majike wanafanana na lava bila viungo hivi (neotenia, Kiing. neoteny). Majike wanakaa katika mdudu ambamo wamezaliwa. Wanatoa kichwa na protoraksi nje ya mwenyeji ili kumrahisishia dume apande jike.

Kuna familia 7 na spishi 110 katika Afrika.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki hariri

  • Xenos zavattarii
  • Corioxenos antestiae
  • Elenchus eastopi
  • Coriophagus zanzibarae
  • Halictophagus clodoceras
  • Halictophagus pontifex
  • Halictophagus regina
  • Halictophagus scheveni
  • Halictophagus zanzibarae

Picha hariri

  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mabawa-potwa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hiyo kuhusu "Mdudu Mabawa-potwa" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.