Mdudu Mabawa-potwa
(Elekezwa kutoka Strepsiptera)
Mdudu mabawa-potwa | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Stylops melittae
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusuoda 2 na familia 12 |
Wadudu mabawa-potwa ni wadudu wadogo wa oda Strepsiptera (strepsis = iliyopotwa, ptera = mabawa) wenye mabawa yaliyopotwa. Wadudu hawa ni wadusia wa wadudu wengine, kama nyuki, nyigu, sisimizi, warukaji-majani, mende, panzi na visamaki-fedha.
Madume ya wadudu hawa wana mabawa, miguu, macho na vipapasio kama wadudu wengine, lakini majike wanafanana na lava bila viungo hivi (neotenia, Kiing. neoteny). Majike wanakaa katika mdudu ambamo wamezaliwa. Wanatoa kichwa na protoraksi nje ya mwenyeji ili kumrahisishia dume apande jike.
Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki
hariri- Xenos zavattarii
- Corioxenos antestiae
- Elenchus eastopi
- Coriophagus zanzibarae
- Halictophagus clodoceras
- Halictophagus pontifex
- Halictophagus regina
- Halictophagus scheveni
- Halictophagus zanzibarae
Picha
hariri-
Picha za Mengenilla moldrzyki zinazoonyesha vipapasio kwa umbo wa uma (juu) na alama za mabawa ya mbele
-
Jike la Stylops melittae akitoa kichwa nje ya mwenyeji
-
Dume la Stylops melittae akipanda jike aliye ndani ya nyuki Andrena vaga
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mabawa-potwa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |