Mdudu Mabawa-makubwa

(Elekezwa kutoka Megaloptera)
Mdudu mabawa-makubwa
Sialis fuliginosa
Sialis fuliginosa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Megaloptera (Wadudu walio na mabawa makubwa)
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusuoda 2 na familia 2:

Wadudu mabawa-makubwa ni wadudu wakubwa kiasi hadi wakubwa sana wa oda Megaloptera (megalos = kubwa, ptera = mabawa) ambao wana mabawa makubwa yakilinganishwa na mwili wao. Wanaruka angani vigoigoi. Muda wa maisha ya wadudu wapevu ni mfupi, kwa kawaida siku chache (si zaidi ya wiki moja). Kwa kinyume lava huishi miaka 1-5 majini.

Oda hii ina familia mbili tu na spishi 8 zimeelezwa katika Afrika. Spishi kubwa kabisa duniani imefunuliwa huko Uchina. Haijapata jina la kisayansi lakini jina la Kiingereza ni Giant dobsonfly. Urefu wa mabawa pamoja ni sm 21.

Spishi za Afrika

hariri
  • Chloroniella peringueyi
  • Leptosialis africana
  • Leptosialis necopinata
  • Madachauliodes ranomafana
  • Madachauliodes torrentialis
  • Platychauliodes capensis
  • Platychauliodes woodi
  • Taeniochauliodes ochraceopennis
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mabawa-makubwa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hiyo kuhusu "Mdudu Mabawa-makubwa" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.