Merlo Silva Albano (alizaliwa mwaka 1979 [1]) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu na mwamuzi wa kimataifa wa nchini Ufilipino.

Maisha ya awali na elimu

hariri

Merlo Silva Albano ni mtoto wa nne wa Loyolo na Mercedes Albano. Alihitimu kutoka chuo cha Holy Cross of Davao College na shahada ya kwanza katika elimu ya viungo

Mpira wa miguu

hariri

Albano alianza kucheza mpira wa miguu mnamo 2004. Katika mwaka huo alichezea timu ya Davao katika mashindano mbalimabli huko Marikina ambapo yalitoa nafasi kwa ajili ya kufanya mazoezi na timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Ufilipino kwa mwezi mmoja. Kisha aliichezea nchi yake kwa mara ya kwanza katika Mashindano ya Wanawake ya AFF 2004 huko Vietnam na pia alicheza katika msimu wa 2007 wa mashindano hayo ambayo yaliandaliwa nchini Myanmar. [2]

Uamuzi

hariri

Akiwa anashirikiana na Chama cha Soka cha Mkoa wa Davao-Kusini cha Shirikisho la Soka la Ufilipino, [3] Albano alikua mwamuzi wa kimataifa wa FIFA mwaka 2012 [4] [5] na kufikia 2018 akawa ni mwamuzi msaidizi anayesimamia mechi za soka la wanawake. Aliongoza katika Kombe la Asia la Wanawake la AFC 2022 . [6]

Marejeo

hariri
  1. "Referees by Association - Philippines". FIFA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Januari 2018. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Indonesia stages miraculous comeback", ASEAN Football Federation, 9 September 2007. Retrieved on 8 January 2018. 
  3. "Davao's Albano in Fifa Refereeing List 2021", Sunstar, 29 January 2021. Retrieved on 3 February 2022. 
  4. "Referees by Association - Philippines". FIFA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Januari 2018. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"Referees by Association - Philippines". FIFA. Archived from the original on January 8, 2018. Retrieved January 8, 2018.
  5. "World-class referee from Davao", Sunstar, 5 April 2019. Retrieved on 3 February 2022. 
  6. "Match official Albano gets WAC appointment". The Philippine Football Federation. 23 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 3 Februari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Merlo Albano kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.