Metsamor (Kiarmenia: Մեծամոր) ni mji uliopo katika Mkoa wa Armavir huko nchini Armenia. Kiwanda cha Umeme wa Nyuklia cha Armenia kinaitwa Metsamor Nuclear Power Plant kipo mjini hapa. Metsamor ilijengwa mnamo mwa 1979 kwa ajili ya nyumba za wafanyakazi wa Metsamor Nuclear Power Plant. Kiwanda hicho cha kuzalishia umeme kilikuja kufungwa mnamo mwaka wa 1989 kwa kufuatia hali ya tetemeko la ardhi ambalo lilipelekea kufungwa kwa kiwanda. Kiwanda hicho kilikuja kufunguliwa tena mnamo mwaka wa 1996 baada ya kuweka vizuizi imara vya tishio la tetemeko la ardhi. Leo hii, kwa haraka-haraka inazalisha umeme wa asilimia 30 mpaka 35 ya mahitaji ya umeme kwa Armenia.

Mji wa Metsamor

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Armenia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Metsamor kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.