Armenia
Armenia (kwa Kiarmenia: Հայաստան Hayastan au Հայք Hayq) ni nchi ya mpakani kati ya Ulaya na Asia katika milima ya Kaukasi iliyoko kati ya Bahari Nyeusi na Bahari ya Kaspi.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kiarmenia: Մեկ Ազգ , Մեկ Մշակույթ "Mek Azg, Mek Mshakowyt" "Taifa moja, utamaduni mmoja" | |||||
Wimbo wa taifa: Mer Hayrenik ("Nchi yetu") | |||||
Mji mkuu | Yerevan1 | ||||
Mji mkubwa nchini | Yerevan | ||||
Lugha rasmi | Kiarmenia | ||||
Serikali | Jamhuri Vahagn Khachaturyan (Վահագն Խաչատուրյան) Nikol Pashinyan (Նիկոլ Փաշինյան) | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa Ilikamilika chanzo cha taifa la Armenia kuanzishwa kwa ufalme wa Urartu kuanzishwa kwa ufalme wa Armenia kupokelewa kwa Ukristo Jamhuri ya Armenia |
23 Agosti 1990 21 Septemba 1991 25 Desemba 1991 11 Agosti 2492 KK 1000 KK 600 KK 301 28 Mei 1918 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
29,743 km² (ya 141) 4.71 | ||||
Idadi ya watu - 2022 kadirio - 2015 sensa - Msongamano wa watu |
3,000,756[1] (ya 1372) 2,974,693 101.5/km² (ya 99) | ||||
Fedha | Dram (AMD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC (UTC+4) DST (UTC+5) | ||||
Intaneti TLD | .am | ||||
Kodi ya simu | +374
- | ||||
1 Maandishi kwa herufi za Kilatini pia "Erevan", "Jerevan" au "Erivan". 2 cheo kulingana na kadirio ya UM ya 2005. |
Imepakana na Uturuki, Georgia, Azerbaijan na Iran. Upande wa kusini kuna eneo la nje la Kiazerbaijan linaloitwa Nakhichevan.
Ingawa kijiografia Armenia huhesabiwa mara nyingi kama sehemu ya Asia, kiutamaduni na kihistoria huhesabiwa pia kama sehemu ya Ulaya.
Jiografia
haririMlima wa kitaifa wa Armenia ni mlima Ararat unaoaminika kuwa mahali ambako safina ya Nuhu ilikuta nchi kavu baada ya gharika kuu inayosimuliwa katika Biblia.
Historia
haririArmenia ni kati ya mataifa ya kale kabisa duniani, ingawa eneo lake limebadilika sana na eneo la sasa ni sehemu ndogo tu ya maeneo yaliyokuwa ya Armenia katika karne na milenia za nyuma.
Armenia ilikuwa nchi ya kwanza ya kupokea Ukristo kama dini rasmi ya kitaifa mnamo mwaka 301. Hadi leo karibu 93% za Waarmenia ni Wakristo wa Kanisa la kitaifa ambalo ni mojawapo kati ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki.
Jambo hilo lilichangia sana mateso yaliyowapata kutoka kwa majirani ambao wengi wao ni Waislamu, hasa Waturuki waliotawala kwa karne nyingi maeneo makubwa ya Dola la Osmani hadi Afrika na Ulaya.
Kilele chake kilikuwa maangamizi ya Waarmenia wakati wa vita vya kwanza vya dunia, ambapo waliuawa zaidi ya milioni moja.
Armenia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti tangu 1920, ikapata uhuru wake tena mwaka 1991.
Kuna fitina na nchi jirani ya Azerbaijan kuhusu eneo la Nagorno-Karabakh linalokaliwa na Waarmenia lakini ni sehemu ya Azerbaijan kisiasa. Mipaka hii ni urithi wa zamani za Umoja wa Kisovyeti. Mara mbili kulikuwa na vita kati ya nchi hizo mbili. Hali halisi Armenia inatawala eneo hili ingawa Nagorno Karabakh ilijitangaza kuwa jamhuri ya kujitegemea isiyokubaliwa na umma wa kimataifa.
Watu
haririWakazi ni hasa Waarmenia asilia (98.1%), halafu Wayazidi (1.2%), Warusi (0.4%) n.k.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiarmenia, ambacho kina alfabeti ya pekee iliyobuniwa na mtakatifu Mesrop mwaka 405 BK.
Upande wa dini, mbali ya Kanisa la kitaifa (92.5%), Wakristo wengine (Waprotestanti na Wakatoliki) ni asilimia 2.3 za wakazi na Wayazidi wanaofuata dini yao asili ni asilimia 0.8.
Matunzio ya picha
hariri-
Yerevan
-
Garni
-
Vagharshapat
-
Khor Virap
-
Sevanavank
-
Khatchkar
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Statistics". Iliwekwa mnamo Machi 17, 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
hariri- (Kiingereza) na (Kiarmenia) (Kirusi) Tovuti ya serikali
- (Kiingereza) Armenica.org - Complete history of Armenia, covering 800 B.C. to 2004
- (Kiingereza) na (Kiarmenia) (Kirusi) PanARMENIAN.Net - Daily Armenian News
- Armenia entry at The World Factbook
- Armenia Archived 11 Juni 2010 at the Wayback Machine. at UCB Libraries GovPubs
- Armenia katika Open Directory Project
- Armenia profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Armenia
- Key Development Forecasts for Armenia from International Futures
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Armenia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Armenia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |