Mia sita sitini na sita

Mia sita sitini na sita ni namba inayoandikwa 666 kwa tarakimu za kawaida na DCLXVI kwa zile za Kirumi.

Ni namba asilia inayofuata 665 na kutangulia 667.

Vigawo vyake vya namba tasa ni: 2 x 3 x 3 x 37.

Matumizi

hariri
  • Namba hurejea miaka 666 KK na 666 BK.
  • Pia humrejea Mpinga-Kristo katika Ufunuo 13:18. Katika nakala nyingi za mstari huo, ndiyo namba ya mnyama[1] ila katika nyingine za zamani, kama vile Papyrus 115, namba yake ni 616.[2] Maelezo yanayokubalika zaidi ni kwamba ndiyo namba ya Kaisari Nero, wa kwanza kudhulumu Kanisa (64-68), kwa kuwa jina lake la Kigiriki likiandikwa kwa herufi za Kiebrania, jumla yake ni 666, na jina lake la Kilatini likiandikwa kwa herufi za Kiebrania, jumla yake ni 616. Hesabu hiyo inawezekana kwa sababu katika Kigiriki na Kiebrania, tofauti na lugha nyingi, hasa za sasa, kila herufi ni pia tarakimu, hivyo ina thamani yake inayoweza kujumlishwa na ile ya herufi nyingine.[3]

Tanbihi

hariri
  1. Beale, Gregory K. (1999). The Book of Revelation: A Commentary on the Greek Text. Grand Rapids, Michigan: Wm. B. Eerdmans Publishing. p. 718. ISBN 080282174X. Retrieved 9 July 2012.
  2. Novum Testamentum Graece, Nestle and Aland, 1991, footnote to verse 13:18 of Revelation, page 659: " -σιοι δέκα ἕξ" as found in C [C=Codex Ephraemi Rescriptus]; for English see Metzger's Textual Commentary on the Greek New Testament, note on verse 13:18 of Revelation, page 750: "the numeral 616 was also read ..."
  3. "666 – professors explain Roulette and Nero in detail; numberphile.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-03-31. Iliwekwa mnamo 2017-03-19.
  Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mia sita sitini na sita kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.