Mianga ya aurora ni mianga ya rangi mbalimbali inayotokea katika matabaka ya juu ya angahewa. Hutazamwa kwa kawaida katika sehemu za Dunia zilizo karibu na ncha ya kaskazini au ya kusini.

Mianga ya aurora.

Kwa Kilatini mianga hiyo ikitokea karibu na ncha ya kaskazini huitwa "Aurora Borealis", ikitokea karibu na ncha ya kusini huitwa "Aurora Australis".

Mianga ya aurora hutokea wakati angasumaku ya Dunia inavurugwa na upepo wa Jua. Inaenea angani wakati wa usiku kwa kilomita mia kadhaa, ikionekana kwa umbali mkubwa. Saa za mchana haionekani kwa sababu haina mng'aro mkali. Mara chache, wakati upepo wa Jua unaongezeka nguvu, mianga ya aurora inaenea pia mbali na ncha hizo kuelekea ikweta.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mianga ya aurora kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.