Ncha ya kaskazini ni mahali pa kaskazini kabisa duniani. Neno hili hutaja ama

Ncha ya Kusini na Ncha Sumaku

Duniani iko kinyume cha ncha ya kusini.

Ncha ya kaskazini ya Kijiografia

hariri

Ncha ya kaskazini ya kijiografia iko katikati ya Bahari ya Aktiki. Ni mahali ambako mhimili wa kuzunguka kwa dunia unagusa uso wa dunia. Mahali hapa papo kwa anwani ya kijiografia ya 90°S na 0°W. Mtu anayesimama hapa anatazama upande wa kusini kwa namna yoyote hata akijizungusha.

Nchani bahari ina kina cha mita 4,087 m. Uso wa bahari umefunikwa hapa na ganda la barafu lenya unene wa mita 3-4. Sakafu ya bahari nchani ulifikiwa mara ya kwanza mwaka 2007 na msafara wa kisayansi wa Urusi kwa kutumia nyambizi.

Mazingira ya ncha ni baridi sana. Eneo lake lenyewe hakuna wakazi wa kudumu watu wa karibu ni Waeskimo wa Greenland na wakazi wa Siberia ya kaskazini (Urusi) pamoja na wanasayansi kwenye vituo vya utafiti.

Usiku na mchana ina muda wa nusu mwaka. Macheo ya pekee hutokea kila mwaka tar. 21 Machi na mchana unaendelea hadi 23 Septemba siku ya machweo. Jua halizami kabisa katika muda huo. Kinachofuata ni machweo na mwanga wa utusiutusi wa wiki kadhaa hadi giza imeanza kabisa inayoendelea hadi Machi.

Kufuatana na kupanda kwa halijoto duniani barafu nchani imeanza kuyeyuka. Wataalamu wengine huamini ya kwamba kuna uwezekano itapotea kabisa katika karne ijayo.

Ncha sumaku ya kaskazini

hariri

Ncha ya kuzunkuka dunia si sawa na ncha sumaku yaani mahali panapoonyeshwa na sumaku za dira dunia. Hapa ni kitovu cha kaskazini cha ugasumaku wa dunia.

Ncha sumaku hutembeatembea kama mwenzake huko kusini. Kwa sasa iko kati ya visiwa vya Kanada na ncha ya kijiografia. lakini iko mahali tofauti kila mwaka.

Nyota ya nchani

hariri

Kuna nyota moja iliyopo moja kwa moja juu ya ncha kwa kurefusha mhimili wa dunia. Nchani huonekana juu kabisa na katikati ya anga. Katika nusu ya kaskazini ya dunia nyota hii ineonekana kote ikionyesha upande wa kaskazini wakati wa usiku. Zamani mabaharia waliweza kutumia nyota hii wakitaka kulenga baharini wakati wa usiku. Kwa lugha ya falaki ni α Ursae Minoris kwa sababu ni nyota ya kwanza katika kundinyota ya Ursus Minor (dubu mdogo). Huitwa pia Stella Polaris (Kilatini kwa nyota ya nchani).

Tazama pia

hariri