Ulanga (madini)

(Elekezwa kutoka Mica)

Kwa matumizi tofauti ya jina hili tazama Ulanga

Mabapa ya ulanga.

Ulanga (kwa Kiingereza: mica) ni kundi la madini yanayopatikana kwa umbo la mabapa membamba. Kikemia ni Madini silikati zinazounda fuwele monokliniki; yaani fuwele zinazoungwa kwenye kona na kujipanga kitabaka; lakini hakuna nguvu ya kushikana baina ya matabaka hayo.

Ulanga ni madini laini yenye ugumu wa Mohs wa 2 pekee.

Huwa na matumizi mengi katika teknolojia elektroniki maana ni kihamiumeme, hutumiwa sana ndani ya kapasita. Ulanga uliosagwa kutumiwa katika ujenzi unaotumia mbao au matofali ya jasi kwa kuziba mapengo (filler).

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ulanga (madini) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.