Michael Mgimwa
Michael Victor Mgimwa (alizaliwa Dar es Salaam, 17 Mei 1993) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Tanzania.
Alianza kucheza mpira akiwa shule ya msingi huko Iringa. Shule hiyo iliitwa Star Internation School. Baadaye akatambuliwa na skauti kutoka Uingereza. Akapata fursa ya kushiriki na Bolto Wanders FC. Chini ya ulezi wa taasisi ya ulezi ya TFF pale Karume.
Alipomaliza elimu ya sekondari pale Jitegemee, akaanza rasmi kujihusisha na mpira mazima. Timu yake ya kwanza kucheza kama mchezaji wa kulipwa ni Moro United na timu ya pili kujiunga ni Mtibwa Sugar FC.[1] Ambapo alishiriki kwenye ligi ya Tanzania msimu wa 2011 — 2012.[2]
Akiwa huko alionyesha umahiri mkubwa wa kulisakata soka huku akishinda magoli 20 katika michuano ya Uhai Cup. Timu yake ya tatu ikawa Roi Et United ya nchini Thailand. Wakati huo ilikuwa daraja la pili. Ilikuwa kati ya 2012—2013. Akaipigania hadi kufikia daraja la kwanza.
Baadaye akajiunga na timu ya Surat Than FC iliyopo kusini mwa Thailand. Ilikuwa ligi ya tatu ambapo alishinda magoli kadhaa yaliyoleta heshima kwa timu. Hiyo ilikuwa kati ya 2013 na 2014.[3]
Mwaka 2015 alirudi Tanzania kushiriki kwenye ligi kuu akaja kuichezea klabu ya African Sport FC ya jijini Tanga kati ya 2015—2016.[4] Akarudi tena Thailand 2017 kwa minajili ya kujiunga na Nan FC na sasa ni mchezaji katika club ya Pow fc ya Thailnda.
Marejeo
hariri- ↑ Oezguer Karatag. "Michael Victor Mgimwa Mtibwa Sugar FC Atacante Listado de Jugadores Jugadores Futbol-Talentos.es". www.futbol-talentos.es. Iliwekwa mnamo 2023-03-24.
- ↑ Anonymous. "MICHAEL VICTOR MGIMWA AOMBEWA ITC THAILAND" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-03-24.
- ↑ "SIMBA SC KATIKA MAZOEZI UDSM JANA, ANGALIA VIFAA VIPYA". BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE. Iliwekwa mnamo 2023-03-24.
- ↑ Unknown (2015-12-24). "KILOWOKO: TFF YAZUIA WACHEZAJI HAWA BAADA YA KUPITIA MAPINGAMIZI YAO". KILOWOKO. Iliwekwa mnamo 2023-03-24.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Michael Mgimwa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |