Michael Owen
Michael Owen (alizaliwa 14 Disemba 1979) ni mchezaji wa soka wa zamani wa Uingereza aliyecheza kama mshambuliaji wa klabu za Liverpool F.C., Real Madrid, Newcastle United, Manchester United na Stoke City; pia alicheza na timu ya taifa ya Uingereza.
Owen alizaliwa katika mji wa Chester na alianza kazi yake kama mwanasoka katika klabu ya Liverpool mnamo mwaka 1996. Aliendelea kucheza kupitia timu ya vijana ya Liverpool na alifunga mwanzoni goli lake la kwanza mnamo Mei 1997.
Katika msimu wake wa kwanza kamili katika Ligi Kuu, alimaliza kama mfungaji bora wa magoli 18. Alirudia hivyo mwaka uliofuata na akawa mfungaji anayeongoza katika klabvu ya Liverpool kuanzia mwaka 1997 hadi 2004.
Kwa kupitia Owen, Liverpool mwaka 2001 ilishinda mataji matatu ya UEFA Champions league, Kombe la FA na Kombe la ligi. Mwaka huo yeye ndiye aliyechukua Ballon d'Or.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Michael Owen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |