Michelle Duppong

Laywoman Mkatoliki wa Marekani

Michelle Duppong (25 Januari 198425 Desemba 2015) alikuwa mwanamke wa Kanisa Katoliki kutoka Marekani ambaye alihudumu kama Mkurugenzi wa Malezi ya Imani kwa Watu Wazima katika Jimbo la Bismarck kabla ya kufariki kwa kansa akiwa na umri wa miaka 31.[1][2]

Awali, alifanya kazi kama mhudumu wa chuo na Fellowship of Catholic University Students (FOCUS), shirika la Kikatoliki kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, katika vyuo mbalimbali katika Midwest ya Marekani.

Tarehe 1 Novemba 2022, Jimbo la Bismarck lilianza mchakato wa kuthibitisha utakatifu wake, na kumuita Mtumishi wa Mungu.[3]

Marejeo

hariri
  1. "U.S. Bishops Affirm Advancement of the Cause of Beatification and Canonization of Servant of God Michelle Duppong | USCCB". www.usccb.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-10-30.
  2. "She lives with Him". Knights of Columbus, Columbia Magazine, page 8 (kwa American English). 2024-04-01. Iliwekwa mnamo 2024-08-11.
  3. "Former FOCUS Missionary Michelle Duppong, Now 'Servant of God,' Continues to Inspire With Her Holy Life". NCR (kwa Kiingereza). 2022-11-14. Iliwekwa mnamo 2023-10-30.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.