Mwiko
Kwa matumizi tofauti ya neno hili angalia Mwiko (kifaa)
Mwiko (Kiing. taboo) ni jambo au au kitu kinachozuiwa mtu kutumia au kutenda kwa kuogopa kudhurika[1].
Dhana ya mwiko hupatikana katika kila utamaduni lakini hutegemea na jamii[2]. Mwiko ni jambo ambalo halikubaliki kuongelea au kufanya. Shughuli au tabia inaweza kuwa mwiko katika utamaduni mmoja, lakini si kwa mwingine.
Baadhi ya mambo kama vile ulaji nyama ya mtu na mahusiano ya kimapenzi kati ya ndugu wa karibu ni mwiko katika jamii nyingi. Wakati mwingine hata kuzungumza juu ya miiko ni mwiko. Kuvunja miiko kunaweza kuonekana kukosa adabu, na kunaweza kusababisha aibu.
Miiko mingi inapatikana katika kanuni za dini mbalimbali, kwa mfano mafundisho ya haramu katika Uislamu au trefe katika Uyahudi.
Marejeo
hariri- ↑ Kamusi ya Kiswahili Sanifu3
- ↑ Taboo - sociology, tovuti ya Encyclopedia Britannica iliangaliwa Septemba 2022