Michael Gerard Tyson (amezaliwa 30 Juni 1966) ni mpiga ngumi wa uzito wa juu duniani unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBC). Ni bondia wa kwanza kuwahi kutwaa taji hilo akiwa na umri mdogo. Mike alizaliwa katika mji wa Brooklyn New York. Alikuwa mtoto mtukutu akijihusisha na matukio ya uporaji mitaani. Alipelekwa katika shule ya kurekebisha tabia (Jela ya watoto) huko New York. Akiwa huko alionekana mwenye kipaji na mwalimu wa ngumi Mmarekani aitwaye Cus D'Amato ambaye matunda yake mengine ni mwanamasumbwi aitwaye Floyd Petterson na kutwaa taji la ngumi 1956.

Mike Tyson (2017)
Mike Tyson (2019)

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mike Tyson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.