Mawougno Mila Ami Aziablé, akijulikana sana kama Mila Aziablé, ni mhandisi na mwanasiasa mwenye asili ya Togo , ambaye alifanya kazi kama waziri kwenye tume ya nishati na madini huko nchini Togo, tangu Oktoba 1 2020.[1]

Asili na Elimu

hariri

Mila ni mzawa wa Togo, aliyezaliwa kijiji cha Circa mnamo mwaka 1991. Alihudhuria elimu ya juu huko Lomé. Kisha akapata nafasi yakujiunga naChuo Kikuu Cha Lomé, kwenye kitengo cha Uhandisi (ENSI).[1]

Kulingana na ufaulu wake mzuri, Mila alizawadiwa nafasi yakusomea masomo ya uhandisi katika chuo cha Metz, huko Ufaransa. Kisha mnamo mwaka 2012, Mila alihitimu nakutunukiwa shahada ya uhandisi wa mekaniki kutoka chuo hicho cha École Nationale d'Ingénieurs de Metz (ENIM), (National Engineering School of Metz), a public engineering school.[1]

Mwaka uliofuata , alijiunga tena na chuo cha Ecole Nationale Supérieure des Mines de Paris (Paris National Superior College of Mines), ikijulikana sana kwa jina la Mines ParisTech. Akiwa chuoni hapo , alijikita sana kwenye masomo ya usimamizi na uhandisi wa gesi .[1]

Mnamo mwaka 2018, alijiunga na chuo cha siasa Paris Institute of Political Studies (Sciences Po), kisha akahitimu na kutunukiwa shahada ya udhamili ya maendeleo na usimamizi wa masuala ya kisiasa .[2]

Baada ya kuhitimu masomo yake , Mila aliajiriwa kama mhandisi msimamizi wa mifumo ya gesi na kampuni ya GRTgaz, ambayo ni kampuni tanzu ya kikundi cha makampuni ya nchini Ufaransa ENGIE.[1][2][3]

Kisha Oktoba mwaka 2020, Mila, akiwa amefikisha umri wa miaka 29 , alipewa cheo cha ujumbe kwa raisi wa jamhuri ya Togo, akijikita kwenye masuala ya Nishati na Madini. Akiwa kama mwanachama mwenye umri mdogo kabisa kwenye tume hiyo . Akichukua nafasi ya Marc Ably Bidamon ambaye alidumu katika cheo hicho tangu mwaka 2015 mpaka mwaka 2020.[1][2][3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 Togo First (4 Novemba 2020). "Mila Aziable: Minister Delegate to the President of the Republic, in charge of Energy and Mines". TogoFirst.com. Lomé. Iliwekwa mnamo 13 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 Togo First (3 Oktoba 2020). "Who is Mila Aziablé, the youngest minister of the new government?". Togoirst.com. Lomé. Iliwekwa mnamo 13 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 Eugène Sahi (12 Aprili 2021). "Togo: Focus on Mila Aziablé, the 29-year-old minister". Afrique-sur7.ci. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-13. Iliwekwa mnamo 13 Septemba 2021. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mila Aziablé kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.