Togo
Togo ni nchi ya Afrika ya Magharibi inayofikia kwenye mwambao wa Ghuba ya Guinea (bahari ya Atlantiki) ikipakana na Benin upande wa mashariki, Burkina Faso kaskazini na Ghana mashariki.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Travail, Liberté, Patrie (Kifaransa: Kazi, Uhuru, Taifa) | |||||
Wimbo wa taifa: Salut à toi, pays de nos aïeux (Usalimiwe nchi ya wazee wetu) | |||||
Mji mkuu | Lomé | ||||
Mji mkubwa nchini | Lomé | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
Serikali | Jamhuri Faure Gnassingbé Victoire Tomegah Dogbé | ||||
uhuru kutoka Ufaransa |
27 Aprili 1960 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
56,785 km² (ya 123) 4.2 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2022 kadirio - 2010 sensa - Msongamano wa watu |
8,492,333 * (ya 102 **) 5,337,000 125.9/km² (ya 93 **) | ||||
Fedha | CFA franc (XOF )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
GMT (UTC+0) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .tg | ||||
Kodi ya simu | +228
- |
Idadi ya wakazi ilikuwa zaidi ya milioni 8 u nusu mwaka 2022.
Jiografia
haririTogo ni nchi ndogo katika Afrika yenye km² 56,785 pekee kwa umbo la pembenne lenye urefu wa urefu wa kilometa za mraba km 550 na upana wa takriban km 130. Mwelekeo wa eneo la nchi ni kaskazini - kusini.
Humo kuna kanda zote za kijiografia za Afrika ya Magharibi kuanzia pwani yenye mchanga na misitu ya minazi kusini, vilima vya nyanda za juu katikati na savana pamoja na maeneo yabisi zaidi ya Sahel kaskazini.
Historia
haririNchi ilianzishwa kama koloni la Togo ya Kijerumani katika pengo kati ya maeneo ya Uingereza na Ufaransa.
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia koloni la Kijerumani liligawiwa kati ya majirani hao kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na baadaye ya Umoja wa Mataifa.
Mnamo Desemba 1956 wakazi wa Togo ya Kiingereza waliamua kwa kura kubaki na Ghana. Hivyo ni Togo ya Kifaransa pekee iliyopata uhuru mwaka 1960.
Rais wa kwanza alikuwa Sylvanus Olympio.
Watu
haririNchini kuna makabila 37; kubwa zaidi ni Waewe (32%). Wazungu hawafikii 1%.
Lugha rasmi ni Kifaransa, ingawa kwa kawaida wakazi wanazungumza lugha za kikabila.
Upande wa dini, mwaka 2020 ilikadiriwa kuwa 47.8% ni Wakristo (hasa wa Kanisa Katoliki) 33% wanafuata dini asilia za Kiafrika na 18.4% ni Waislamu (hasa Wasuni).
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- Bullock, A L C, Germany's Colonial Demands (Oxford University Press, 1939).
- Gründer, Horst, Geschichte der deutschen Kolonien, 3. Aufl. (Paderborn, 1995).
- Mwakikagile, Godfrey, Military Coups in West Africa Since The Sixties (Nova Science Publishers, Inc., 2001).
- Packer, George, The Village of Waiting (Farrar, Straus and Giroux, 1988).
- Piot, Charles, Nostalgia for the Future: West Africa After the Cold War (University of Chicago Press, 2010).
- Schnee, Dr. Heinrich, German Colonization, Past and Future – the Truth about the German Colonies (George Allen & Unwin, 1926).
- Sebald, Peter, Togo 1884 bis 1914. Eine Geschichte der deutschen "Musterkolonie" auf der Grundlage amtlicher Quellen (Berlin, 1987).
- Seely, Jennifer, The Legacies of Transition Governments in Africa: The Cases of Benin and Togo (Palgrave Macmillan, 2009).
- Zurstrassen, Bettina, "Ein Stück deutscher Erde schaffen". Koloniale Beamte in Togo 1884–1914 (Frankfurt/M., Campus, 2008) (Campus Forschung, 931).
Viungo vya nje
hariri- Serikali
- (Kifaransa) Republic of Togo official site
- (Kifaransa) National Assembly of Togo Ilihifadhiwa 11 Mei 2011 kwenye Wayback Machine. official site
- Chief of State and Cabinet Members Ilihifadhiwa 10 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Taarifa za jumla
- Country Profile from New Internationalist
- Country Profile from BBC News
- Togo from Encyclopaedia Britannica
- Togo entry at The World Factbook
- Togo Ilihifadhiwa 7 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Togo katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Togo
- Key Development Forecasts for Togo from International Futures
- Vyombo vya habari
- (Kifaransa) Web Radio Togo Ilihifadhiwa 17 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine. official Web Radio
- Biashara
- Utalii
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Togo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |