Sukulenti (lat. sucus = utomvu; ing. succulents) au Mimea yenye utomvu mwingi ni mimea iliyojitohoa kwa maisha katika mazingira yabisi.

Jani la mshubirimani lililokatwa; utomvu unatoka nje

Mimea hii ya familia na jenasi tofauti ina uwezo wa kutunza maji ndani ya majani au mashina yao. Kwa hiyo mara nyingi ama majani au shina ni nono kutokana na uwingi wa utomvu ndani yao.

Kwa hiyo "sukulenti" si jina la spishi au familia maalumu ya mimea lakini neno hili linataja tu umbo la mimea ya aina mbalimbali iliyo imekuwa tofauti kutokana na mazingira yake. Jenasi moja ya mimea inaweza kutia ndani aina zenye majani nono yenye utomvu mwingi na pia aina nyingine zenye majani ya kawaida zinazomea katika mazingira tofauti.

Pia kuna tofauti kati ya watalaamu eti ni nini inayostahili kuitwa sukulenti. Wengi wanaangalia majani na mashina pekee lakini kuna wengine wanaoingiza mle pia mizizi inayotunza maji lakini wengine hawakubali.

Mifano ya sukulenti iliyokubalika na pande zote ni mbuyu, mkonge, mshubirimani na aina za mpungate.

  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sukulenti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.