Minara ya ziwa Jumeirah

Huchangia maendeleo makubwa huko Dubai, Falme za Kiarabu

Minara ya ziwa Jumeirah (Kiarabu ابراج بحيرة الجميرا) ni eneo kubwa la maendeleo huko Dubai, [United Arab Emirates] ambalo lina majumba 79 yalinayojengwa kando mwa maziwa, Manne ya kutengenezwa na binadamu (Ziwa Almas Magharibi, Ziwa Almas Mashariki, Ziwa Elucio, na Ziwa Allure) vile vile, kuna jumba la JLT la 8 linalotazamana na visiwa vya Jumeirah. Maziwa haya (ambayo ni mita 3 kwenda chini) maziwa haya yalijazwa kabisa mwisho wa mwaka 2009. [1] Jumla ya eneo lililofunikwa na maziwa, njia ya maji na ardhi itakuwa mita za mraba 730,000. Majumba yatakuwa na maghorofa mbalimbali, kutoka 35 hadi 45, isipokuwa lile la kati ambalo litakuwa na ghorofa 66. Jumba refu kabisa na lile maarufu kabisa katika eneo hili litakuwa [Almas Tower] ambalo litakuwa katika kisiwa chake pekee kati ya Ziwa Almas Magharibi na Ziwa Almas Mashariki. Majumba yote ya makazi yatakuwa katika makundi matatu. Hili litarahisisha usambazaji wa barua.

Ukamilishaji wa mnara wa Saba mwezi Desemba 2006 uliadhimisha jumba la kwanza kukamilika katika minara ya ziwa Jumeirah. Jumba la mwisho linatarajiwa kukamilika mwaka 2011. Ujenzi kwa kiasi kikubwa ulifinyika mwaka 2008.

Mwezi Oktoba mwaka 2008 jumla ya majumba 19 yalikuwa tayari kutumika na mengine 6 yalifunguliwa mwishoni mwa mwaka 2008.

Tarehe 18 Januari mwaka 2007, wafanyakazi wawili waliuawa na wengine wapatao 40 kujeruhiwa wakati moto ulipozuka katika ujenzi wa chini wa mnara Fortune. [2] Ujenzi wa mnara wa Fortune ulisimamishwa kwa miezi kadhaa, lakini ulitarajiwa kukamilika mwishoni mwaka 2007.

Vichala

hariri

Majumba katika JLT yamepangwa katika makundi ishirini na sita (26), kila moja majumba matatu, na yamepewa majina kutoka A hadi Z, kila mnara kuna eneo lake la maegesho na duka la rejareja. Majumba hayo yana majina 1, 2, 3 lakini pia yana majina rasmi. Vichala havina majina rasmi.

Hoteli

hariri

Hoteli nne zitajengwa katika mradi huu, Mövenpick Hoteli katika kiwanja namba A2, Bonnington katika minara ya ziwa ya Jumeirah katika kiwanja namba J3, na hoteli zisizojulikana katika viwanja T3 na z2; kutakuwa pia na majumba ya makazi ya ghorofa.

Al Mas na Biashara ya Madini

hariri

Jumba kuu ni jengo la Al Mas (Kiarabu: "ya Diamond") na hili ni makao makuu ya DMCC pia na Mabadilishano ya almasi za Dubai. Wamiliki na wapangaji wote ni mafanyibiashara wa almasi. Upande wa chini wa jumba hili ndipo hifadhi ya almasi ilipo.

Majumba mengine yanayomilikiwa na DMCC, Au na Ag, yatakuwa makazi ya Mabadilishano ya dhahabu Dubai na Mabadilishano ya shaba mfululizo na pia litakuwa na wanachama wa DMCC pekee.

Idadi ya Watu na Vifaa

hariri

Mradi huu unakadiriwa kuwa na wakazi wapatao takribani 60,000 na wanaokuja kufanya kazi ni 120.000; utakuwa na nyanja 5 za kucheza za watoto, misikiti 3, kituo cha polisi, kituo cha ulinzi wa kiraia na vifaa vingine.

Kutakuwa na vituo viwili vya reli za mwanga za Dubai na basi kutoka vichala kwa vituo hivi vya Reli vimepangiwa.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons


  1. [2] ^ Ukweli wa Jumeirah Lake Towers Archived 25 Januari 2009 at the Wayback Machine.
  2. [3] ^ Wafanyakazi kufa katika moto wa jumba la Dubai - [BBC News] - zilizopatikana tarehe 18 Januari 2007.