Minyoo Mchanga (Sandworm – huitwa pia Nereididae, ragworm, na clam worm) ni minyoo wanaoishi sehemu ya chini ya ardhi. Mashimo haya ni yenye miundo mfano wa herufi I, J, U na Y.[2] Minyoo-Mchanga huishi kwenye mashimo kwa maisha yao yote. Hutumia kamasi wao kujenga mashimo yalio imara.[2]

Picha ya Nereis virens, spishi ya Minyoo-Mchanga
Himaya: Animalia
Faila: Annelida
Clade: Pleistoannelida
Ngeli chini: Errantia
Oda: Phyllodocida
Oda chini: Nereididaeformia
Familia: Nereididae
(Fauchald, 1977)[1]

Minyoo-Mchanga huishi duniani kote. Wengi huishi katika maji chumvi ya bahari, lakini hupatikana katika mawimbi na ardhi ya baharini, ndani ya maji katika mashimo ya miti, na katika mapango pia. Huishi pia katika maeneo ya viumbe wa sakafu ya bahari (benthos) na karibu na nyufa za majimoto zilizoko katika sakafu ya bahari (haidrothermal vents).[3] Minyoo-Mchanga hupatikana kwa wingi zaidi katika bahari ya Ulaya na mazingira ya fyordi (fjord).[4] Pia hupatikana katika bahari ya Kanada na Brazil.[2][5]

Vyakula

hariri

Minyoo-Mchanga ni walachochote (omnivore). Hii inamaanisha wao hula vyakula vya aina zote. Minyoo-Mchanga hula vidubini au mabaki ya wanyama wa bahari. Minyoo-Mchanga hula mimea ya baharini na wanyama wadogo pia. Wakati wanajenga mashimo, Minyoo-Mchanga hula udongo. Minyoo-Mchanga hula madini, udongo, mchanga, miamba, na vitu vingi vya ardhi chini ya bahari.[4]

Vyakula ambavyo Minyoo-Mchanga hula husababisha kuwa na meno magumu miongoni mwa minyoo. Meno ya Minyoo-Mchanga hutengenezwa kwa zinki nyingi na amino asidi ambayo ni histidini na glaisini.[6]

Kwa sababu Minyoo-Mchanga hula ardhi na madini, hivyo huwa ni muhimu kwa sayansi ya wanyama na uchafuzi wa bahari. Uchimbaji wa madini baharini huacha madini kwenye eneo la bahari, kwa viumbe hai wa baharini. Madini haya husababisha wanyama au viumbe hawa kuumwa. Lakini wanyama kama Minyoo ya Polikit (polychaete), Minyoo-Mchanga, wanaweza kula madini. Wanasayansi hutumia Minyoo-Mchanga kupata ufahamu kuhusu wanyama wa baharini, jinsi wawezavyo kuishi katika madini na uchafuzi wa mazingira.[4]

Sehemu

hariri
 
Uso na koromeo ya Nereis, genus ya Nereididae[6]

Sehemu ya kwanza ya Mnyoo-Mchanga inakuwa na minyiri (mikono), na mdomo mkali. Inakuwa na macho pia. Sehemu ya pili ya Mnyoo-Mchanga inakuwa na minyiri (mikono) minne kama nywele ndogo kwenye vijasumu lakini kubwa sawa na urefu wa Mnyoo-Mchanga. Sehemu inayofuata ni minyiri (mikono) tu.[7] Minyoo-Mchanga inaweza kuwa na sehemu hadi laki mbili.[7] Minyoo-Mchanga huwa na rangi tofauti tofauti (Alitta virens rangi ya kahawia, nyekundu kali, au kijani kali).[7]

Katika sehemu za Mnyoo-Mchanga, kuna mifumo ya damu ya kutosha mwili wa mnyoo. Hakuna seli za kutengeneza ukuta wa mishipa kuweza kukinga na kuzuia damu, lakini damu hupita kwenye nafasi kati ya viungo vidogo. Damu hutumia mishipa midogo kutoka mishipa karibu na uti wa mgongo mpaka mishipa mbele ya uti wa mgongo.[3]

Minyoo-Mchanga huzaa mara moja katika maisha yao (semelparous) na hawana wenza maalumu (promiscuous). Nereididae hupata watoto mara moja tu katika maisha yao. Wakati wa kuzaa watoto, sehemu ya mwisho hushiba mayai au manii. Madume na majike huogelea juu ya mashimo. Majike hutaga mayai juu ya maji ya bahari. Majike huwa yanakufa baada ya kutaga mayai. Madume humwaga manii juu ya mayai. Mayai yenye manii hufunguka kutoa watoto.[7]

Marejeo

hariri
  1. Read, G.; Fauchald, K. (Ed.) (2024). World Polychaeta Database. Nereididae Blainville, 1818. Accessed through: World Register of Marine Species at: https://marinespecies.org/aphia.php?p=taxdetails&id=22496 on 2024-10-18
  2. 2.0 2.1 2.2 Salvo F, Dufour SC, Archambault P, Stora G, Desrosiers G. Spatial distribution of Alitta virens burrows in intertidal sediments studied by axial tomodensitometry. Journal of the Marine Biological Association of the United Kingdom. 2013;93(6):1543-1552. doi:10.1017/S0025315413000519
  3. 3.0 3.1 Wilson, R.S. (2000) Family Nereididae. In Beesley, P.L., Ross, G.J.B. and Glasby, C.J. (eds) Polychaetes and allies: the southern synthesis. Melbourne: CSIRO Publishing, pp. 138-141.
  4. 4.0 4.1 4.2 Anne Mette T. Simonsen, Kristine B. Pedersen, Pernille E. Jensen, Bo Elberling, Lis Bach, Lability of toxic elements in Submarine Tailings Disposal: The relationship between metal fractionation and metal uptake by sandworms (Alitta virens). Science of The Total Environment, Volume 696, 2019, 133903, ISSN 0048-9697, https://doi.org/10.1016/j.scitotenv.2019.133903. (https://www.sciencedirect.com/science/article/pii/S0048969719338537)
  5. Amaral, A.C.Z.; Nallin, S.A.H.; Steiner, T.M.; Forroni, T. O. & Gomes, D. F. 2006-2012. Catálogo das espécies de Annelida Polychaeta do Brasil. http://www.ib.unicamp.br/museu_zoologia/files/lab_museu_zoologia/Catalogo_Polychata_Amaral_et_al_2012.pdf (consultado em 18/10/2024).
  6. 6.0 6.1 Broomell, Chris C. and Chase, Sue F. and Laue, Tom and Waite, J. Herbert, Cutting Edge Structural Protein from the Jaws of Nereis virens. Biomacromolecules, 2008;9(6):1669 1677. doi: 10.1021/bm800200a
  7. 7.0 7.1 7.2 7.3 Britannica, The Editors of Encyclopaedia. Rag Worm. Encyclopedia Britannica, 12 Feb. 2018, https://www.britannica.com/animal/rag-worm. Accessed 14 October 2024.
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Minyoo-Mchanga kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.