Mkoa wa Plateaux, Togo

Mkoa wa Plateaux ni mojawapo ya mikoa mitano ya Togo. Plateaux iko kaskazini kwa Mkoa wa Maritime na kusini kwa Mkoa wa Kati (Centrale).

Hifadhi ya msitu wa Deux Bena iko kwa kimo cha mita 800 kwenye Mkoa wa Plateaux
Mkoa wa Plateaux
Mikoa ya Plateaux

Upande wa magharibi mkoa unapakana na Ghana na upande wa mashariki unapakana na Benin.

Jina "Plateaux"[1] linamaanisha nyanda za juu. Mlima Agou (mita 986) ni sehemu ya juu zaidi nchini Togo.

Mkoa huo una eneo la kilomita za mraba 16,975. Plateaux ni mkoa mkubwa zaidi kieneo na ina idadi ya pili ya wakazi baada ya Mkoa wa Maritime kwa sababu mwaka 2020 walikadiriwa kuwa 1,705,300.[2]

Makao makuu ya mkoa yako mjini Atakpame.

Miji mingine mikubwa katika eneo la Plateaux ni pamoja na Kpalime na Badou.

Plateaux imegawanywa katika wilaya za Agou, Amou, Danyi, Est-Mono, Haho, Kloto, Moyen-Mono, Ogou na Wawa.

Marejeo

hariri
  1. tamka "platoo"
  2. https://www.citypopulation.de/en/togo/cities/ Togo, Regions; tovuti ya citypopulation.de