Mkoa wa Thiès ni mkoa mmojawapo nchini Senegal. Makao makuu yako mjini Thiès. Mkoa una eneo la kilomita za mraba 6,670 linalokaliwa na wakazi 1,788,864 [1].

Mahali pa Mkoa wa Thies nchini Senegal
Wilaya za mkoa wa Thies

Jiografia hariri

Mkoa una maeneo mawili ya pwani, moja upande wa kaskazini kwenye Grande Côte (pwani kubwa) penye soko la mboga la Niayes, na moja upande wa kusini kwenye Petite Côte (pwani ndogo) ambayo ni moja ya maeneo ya kitalii ya Senegal.

Mkoa huu unazunguka Rasi ya Cap-Vert yenye mji mkuu Dakar, hivyo reli na barabara kuu za nchi zinapita mkoani.

Wilaya hariri

Mkoa wa Thiès umegawanywa katika wilaya 3 (departements):

Marejeo hariri

  1. https://www.citypopulation.de/en/senegal/admin/ Senegal: administrative divisions

Viungo vya nje hariri