Mlango wa Tiran ni mlangobahari baina ya Rasi ya Sinai (Misri) na Rasi ya Uarabuni (Saudia). Inaunganisha Bahari ya Shamu (Red Sea) na Ghuba ya Aqaba.

Ramani ya Mlangobahari wa Tiran
Mlangobahari wa Tiran kwa macho ya satelaiti

Jina lilitokana na kisiwa kidogo cha Tiran kilichopo katikati ya mlangobahari. Sehemu hii ni muhimu kwa sababu ni

Kwenye kaskazini ya Ghuba ya Aqaba kuna mabandari mawili ya Eilat (Israel) na Aqaba (Jordani) yanayotegemea njia ya Tiran.

Vita ya 1967

hariri

Mwaka 1967 wakati wa uadui mkali baina ya Misri na Israel rais wa Misri Jamal Abd al Nasser aliamua kuzuia usafiri wote kuja na kwenda Eilat. Hatua hii ilitazamiwa na Israel kama tangazo la vita[2] ikasababisha Vita ya Siku Sita ambako Israel ilishinda mataifa majirani ya Waarabu na kutwaa Sinai yote kwa miaka iliyofuata pamoja na kisiwa cha Tiran. Tangu amani ya mwaka 1979 baina ya Misri na Israel eneo lilirudishwa kwa Misri iliyoahidi kutunza mpito huria kwa meli za mataifa yote.

Mipango ya daraja juu ya mlangobahari

hariri

Tangu mwaka 1998 kuna mipango kujenga daraja juu ya mlangobahari itakayounganisha Misri na Saudia[3]. Mipango hii iliahirishwa mara kadhaa kutokana na wasiwasi juu ya athira ya mazingira na pia wasiwasi upande wa Israeli kuhusu usalama wa njia ya bahari. Mwaka 2016 mfalme wa Saudia alitangaza tena ya kwamba Saudia iko tayari kugharamia daraja na kuanzisha ujenzi.[4]

Marejeo

hariri
  1. Israel ina pia mabandari upande wa Bahari ya Mediteranea
  2. 26 Statement to the General Assembly by Foreign Minister Meir- 1 March 1957, tangazo la Waziri wa Mambo ya Nje ya Israel mbele ya Umoja wa Mataifa mwaka 1957, tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, ilitazamiwa Juni 2018
  3. Egypt Approves Massive Bridge to Saudi Arabia, tovuti ya Der Spiegel, July 18, 2011, iliangaliwa juni 2018
  4. Saudi Arabia and Egypt announce Red Sea bridge, tovuti ya BBC, 8 April 2016, iliangaliwa Juni 2018