Mlanyoka

ukarasa wa maana wa Wikimedia
Mlanyoka

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Fitzinger, 1843
Nusufamilia: Aparallactinae (Nyoka wanaofanana na matandu)
Bourgeois, 1968
Jenasi: Polemon
Ngazi za chini

Spishi 13:

Walanyoka ni nyoka wenye sumu wa jenasi Polemon katika familia Lamprophiidae. Wamepewa jina hili kwa sababu hula nyoka wengine wadogo kuliko wao wenyewe.

Nyoka hawa sio warefu sana, sm 85 kwa kipeo. Kichwa hakina shingo na mkia ni mfupi sana wenye ncha kama msumari. Rangi yao ni nyeusi au kahawia iliyoiva sana. Kichwa au kisogo kinaweza kuwa cheupe, njano au hudhurungi.

Walanyoka huishi katika vishimo au chini ya takataka za majani ambapo huwinda nyoka wengine.

Chonge ni meno ya nyuma na zina mitaraza. Wakishikwa na mtu hawawezi kuingiza sumu yao. Kwa hivyo nyoka hawa sio hatari.

Spishi

hariri

Marejeo

hariri
  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mlanyoka kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.