Vesuvio
(Elekezwa kutoka Mlima Vesuvio)
Vesuvio ni volkeno nchini Italia. Iko karibu na jiji la Napoli.
Ni volkeno hai iliyoendelea kuwa na milipuko mara kwa mara tangu mlipuko wake wa kwanza iliyojulikana mwaka 79 BK.
Leo hii inaonekana kuwa ni volkeno yenye hatari sana kwa sababu baada ya muda bila milipuko mikubwa mazingira yake yamejaa watu katika eneo la jiji la Napoli, takriban milioni tatu.
Ilipolipuka mwaka 79 BK iliharibu miji ya Pompei na Herkulaneo ikaua watu maelfu. Mlipuko huu una maarufu kwa sababu mwandishi Mroma Plinio aliutazama akaandika taarifa juu yake. Miji miwili iliyofunikwa na majivu ya Vesuvio ilifunuliwa tena katika karne ya 20 imetupa picha nzuri ya maisha ya Kiroma ya kale.